Alhamisi, 16 Julai 2015
MAMBO MAWILI(2) MUHIMU ILI KUPEWA KIBALI CHA KUJENGA JENGO
Je Umeipenda Hii Habari?
Kabla ya yote bonyeza maandishi ya bluu hapo chini ili kusoma habari zilizokwisha wekwa ambazo zinaweza kukusaidia
vitu vya kuchunguza kabla hujanunua kiwanja
Kabla hujafikiria kujenga zingatia haya
Vitu 11 vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali
Hatua za kufuata ili
kupewa kibali cha kujenga jengo.
Kwanza kabisa wanaotoa
kibali cha kuruhusu jengo lijengwe ni mamlaka za kiserikali za eneo husika hasa
manispaa, kwa maana wao wanao ramani ya mji mzima inayoonesha mipangilio ya aina
za majengo yanayotakiwa kujengwa katika kila mtaa.
1. Hati halali ya eneo – Hii
hasa kwa wale wanaotaka kujenga majengo ya gholofa na ya kibiashara ni lazima
kuhakikisha unakuwa na hati halali inayoonesha kwamba sehemu unayotaka kujenga
ni mali yako.
mfano wa hati ya kiwanja
2. Michoro kamili na iliyowekwa
muhuri – hii ni ile ya msanifu majengo(architectural drawings) kwa majengo ya
kawaida ya kuishi(residential) ya chini (one storey) kwa yale ya ghorofa pia
itahitajika michoro ya mhandisi majengo(structural drawings), mhandisi umeme
(electrical drawings), na michoro ya mfumo wa maji safi na taka
(plumbing).
Kumbuka :
michoro hii yote inatakiwa iwe imepigwa muhuri ili kuonesha kwamba imechorwa na
wataalamu wenye sifa na wanaotambulika.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
usiache kuweka neno hapo
chini
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
1 COMMENT
23 Septemba 2020, 01:26
HABARI MIMI NIMEKUTANA NA CHANGAMOTO MOJA -KIWAJA CHANGU NIMEPIMA NASUBIRI HATI,NIKAANZA UJENZI NIKASIMAMISHWA NA MTU FULANI AKANIAMBIA SINA KIBALI CHA KUJENGA ,AKANIAMBIA ANATOKEA KWA MWENYEKI MTENDAJI WA MTAA,HIVYO NIFIKE CHA AJABU WAKANIAMBIA NILIPE KIASI FULANI BILA KUPEWA CHOCHOTE CHA UTHIBITISHO KWA AHADIYA KULINDWA HADI NIMALIZE UJENZI,NIKATOA NUSU LAKINI NINA WASIWASI SANA KAMA NI NJE YA UTARATIBU,NA KWA MUJIBU WA MAELEZO YENU MIMI BADO SINA HATI NA NAHITAJI KUENEDELEA NA UJENZI KIDOGO KIDOGO WA NYUMBA YA KUISHI YA ROOM 3,JE NIFANYEJE ILI KUPATA LIBALI HALALI-0714-49-31-51 NAMBA YANGU KWA MSAADA ZAIDI,
Chapisha Maoni