+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumatatu, 3 Novemba 2014

Hii ndiyo orodha ya watu wanaohusika kukamilisha kazi za ujenzi (building team)

   mpendwa msomaji wa makala hizi zinazohusu ujenzi, hapo chini utaona orodha ya watu wanaohusika na ujenzi kwanzia mwanzo mpaka mwisho pamoja na majukumu yao.

pic 1
1. Mteja/mwajiri
huyu ndio mtu au watu wa msingi katika ujenzi ambaye ndiye mhitaji wa jengo, mmiliki wa kiwanja, na mwezeshaji au mwekezaji wa jengo. mteja/mwajiri anaweza kuwa mtu, kikundi cha watu, idara, asasi, au serikali.
Mwajiri/mteja sio lazima awe na ufahamu wa maswala ya ujenzi
2. Timu ya wabunifu
Hawa ni watu wenye ujuzi wa ubunifu katika ujenzi wanaohusika na utengenezaji wa muonekano wa jengo na uandaaji wa mpango kazi. Timu ya wabunifu huwa na wabunifu wa aina tofauti kama msanifu majengo(architect), mkandarasi wa majengo( structural engineer) na wengineo. (tutawaelezea vizuri katika makala zijazo).
3. Msimamizi wa majengo(clerk of work)
Huyu ni mmoja wa wahusika katika timu ya ujenzi anayeajiliwa na mteja/mwajiri kwa lengo la kuhakikisha kwamba kontrakta (contractor) anajenga jengo kulingana na michoro ya jengo.
4. Timu ujenzi (construction team)
Hii ni timu inayowajibika kujenga jengo kulingana na mawazo na michoro kutoka kwa wabunifu kwa kuzingatia ubora, viwango, usalama, na uchumi uliopo. Timu hii pia inaunganisha watu wenye utaalamu tofauti tofauti kama mkadiriaji, mnyapara (foreman) na wengine wengi. (tutawaelezea vizuri kwenye makala zijazo).
5. Mgawaji/mletaji (supplier)
Huyu anahusika na kuleta/ kupeleka mahitaji kama cement, vigae, mchanga na vitu vingine vinavyohusu ujenzi eneo la ujenzi.
6. Mdhibiti/mrekebishaji (regulator)
Huyu anahusika na kulinda watumiaji wa jengo na wafanyakazi dhidi ya njia mbaya za ujenzi.
kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwenye email ujenzielekezi04@gmail.com
usisahau kuweka neno hapo chini

Jumatano, 8 Oktoba 2014

Vitu kumi na moja (11) vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali cha ujenzi


Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya kuwa na seti ya michoro ya jengo (architectural drawings), hivyo basi kuna vitu vya kuzingatia na ambavyo vinatakiwa kuwepo kwenye michoro hiyo ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza wakati ukitafuta kibali cha kujenga jengo.
Vitu hivyo ni;
1.    Namna jengo litakavyokuwa (plans section, elevation, foundation and roof plan)
Ili kupata kibali cha ujenzi lazima kuwe na michoro itakayoonesha msingi(foundation) utakavyokuwa, mchoro wa kipande/sehemu ya jengo(section plan), paa, na mionekano ya mbele, nyuma, kushoto, na kulia. Michoro yote hii ya namna jengo litakavyokuwa inatakiwa iwe na vipimo vinavyoonekana vizuri.

Mchoro wa jengo (floor plan)

Mchoro wa sehemu ya jengo(section plan)

Mchoro wa paa (roof plan)

Mchoro unaoonesha mionekano ya jengo (elevation)


2.    Namba na eneo la kiwanja kilipo
Hivi huonekana sehemu ya chini au kulia Katika michoro ya namna jengo litakavyokuwa.


3.    Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
Pia sehemu hii huonekana katika michoro yote ya jengo upande wa kulia au chini.

4.    Jina la mchoraji na anwani
Pia hii sehemu huonekana chini au kulia katika michoro ya jengo.


5.    Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
Hii sehemu huonekana kwenye mchoro wa jengo(floor plan) au kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya kiwanja na jengo (site plan).


6.    Ujazo wa kiwanja (plot coverage)
Hii sehemu hueleza ujazo utakao chukuliwa na jengo katika kiwanja, pia huonekana kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya jengo na kiwanja(site plan).


7.    Uwiano (plot ratio)
Hii sehemu hueleza uwiano kati ya jengo na kiwanja, pia huonekana katika mchoro wa site plan.


8.    Matumizi yanayokusudiwa
Hii sehemu hueleza kusudio la matumizi ya jengo, pia huonekana kulia au chini katika michoro yote ya jengo.

9.    Idadi ya maegesho yatakayokuepo
Hii sehemu huonesha idadi ya maegesho ya magari na vitu vingine vinavyozunguka jengo ndani ya kiwanja husika, pia huonekana katika mchoro wa site plan.


10. Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
Hii sehemu hutumika kuonesha umbali uliopo kutoka katika mipaka ya kiwanja mpaka jengo husika, pia huonekana kwenye mchoro wa site plan.


11. Mfumo wa kutoa majitaka hadi kwenye mashimo
Hii sehemu huonesha jinsi ya kutoa majitaka kutoka kwenye jengo mpaka kwenye mashimo ya kuhifadhia,pia sehemu hii huonekana kwenye site plan.


Kutokana na maelezo hapo juu, kwa mtu yeyote anayehitaji kujenga jengo inabidi ahakikishe kila kitu nilichokielezea hapo juu kinaonekana katika seti ya michoro ya jengo (architectural drawings) kabla ya kuendelea na utaratibu mwingine unaofuata.
Kwa maelezo Zaidi wasiliana nami kwenye email; ujenzielekezi04@gmail.com
Usisahau kuweka neno hapo chini

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506