+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumanne, 14 Julai 2015

VIFAA 12 VYA MSINGI KUWANAVYO FUNDI BOMBA (PLUMBER)


Habari za wakati mpendwa msomaji! katika mada hii tunataka tukupitishe kwenye mambo yahusuyo vifaa vya kiufundi. Hii ni kwa ajili ya wewe fundi unaetaka kuanza shughuli(kujitegemea), au wale watu wanaotaka kuanzisha kamradi kadogo, na pia hata kwa wale watu wanaopenda viwepo majumbani kwao kwaajili ya mambo ya dharura au kupunguza makali ya gharama za kiufundi.

VIFAA VYA MSINGI KWA MAFUNDI BOMBA(PLUMBING)
1. Koleo (tongue & groove pliers) – kazi yake ni kukaza, kulegeza na kuvuta kipande cha bomba(connector) au nati. zipo za nchi 10 na nchi 12.

2. msumeno (hacksaw) – kazi yake ni kukata vipande vya bomba na nati.

3. kinoleo (metal file) – kazi yake ni kunoa (kurudisha makali) ya mabomba ya metali.

4. Basin wrench – kazi yake ni kukaza na kulegeza nati.

5. pipe wrench – hii pia hutumika kukazia na kulegeza nati ndogo zaidi na za ukubwa tofauti.

6. Adjustable wrench – kazi yake ni kubana sehemu zinazohitajika kubana kama kwenye baadhi ya sehemu zilizoungana (connector)

7. Propane torch – hili ni dumu/kidumu kilicho na gesi, kazi yake ni kuyeyusha mabomba hasa mabomba ya kopa sehemu za kuunganishia.

8. Hand auger – kazi yake ni kusafisha sink, tube na mabomba.

9. Tubing cutter – kifaa hiki kinatumika kwa kukata kwa urahisi mabomba hasa hasa mabomba ya kopa.

10. Plunger – kazi yake ni kutoa uchafu kwenye vyoo, bafu na sink.

11. Closet auger – kazi yake ni kusafisha sehemu za ndani za mabomba sink, vyoo nk.

12. koti gumu (overall) – kazi yake ni kujikinga na moto, vitu vichafu na kuwa salama kiafya.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
usiache kuweka neno hapo chini
 

3 COMMENTS

mohamedy luzayger alisema ...
9 Januari 2022, 00:54

Asanten kwa kutuletea kulasa hii kwa si ambao ndio tunaingia katka fani mbalikiwe


Bila jina alisema ...
15 Julai 2022, 03:21

Asanteh kwa maoni na maelekezo lakini je nikiwa nahtaji


Bila jina alisema ...
30 Januari 2023, 10:37

Asanten naomben anaejua ppf ya kuhusu mabomba Kwan anejua


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506