Jumamosi, 25 Julai 2015
LIFAHAMU BAFU MVUKE (SAUNA)
Je Umeipenda Hii Habari?
Karibu sana mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi. Leo tunaendelea na mfululizo wa makala zetu za ujenzi kama ilivyoada.Leo tunaangazia kuhusu Sauna au Bafu mvuke. Huenda ulishawahi kusikia kuhusu hili neno au kupata kutumia kabisa chumba hiki.Sauna huweza kujengwa nje ya jengo kuu au likawa ndani ya jengo kuu.
Sauna au ( Bafu la mvuke kwa Kiswahili ) ni Chumba kidogo au jengo lililosanifiwa / buniwa kama sehemu ya kupata joto la mvuke. Mvuke ambao huweza kuwa mkavu au wenye maji maji.
Ambapo mvuke na joto la hali ya juu huwafanya watu kutoka jasho.
Sauna huweza kugawanyika katika Makundi mawili.
1.BAFU MVUKE LA KAWAIDA / ASILI :
Hii ni sauna ambayo huipa hewa joto na kisha hewa kusambaa katika chumba na kuipasha ngozi.Sauna hii hupitisha joto kwa njia ya uoevu (convection).
2.BAFU MVUKE LA MIALI:
Hii ni sauna ambayo hupasha vitu joto moja kwa moja.
Bafu mvuke la miali hutumia nyenzo mbali mbali kwa ajili ya kupasha joto kama vile mkaa, nyuzi nyuzi hai za kaboni na nyenzo nyingine nyingi.
UTENDAJI KAZI WA SAUNA:
Jotoridi ambalo hukaribia 100oc (212o F) Litakuwa moja kwa moja halivumiliki kabisa.
Sauna huwekewa madirisha madogo kiasi yenye matundu ambayo huruhusu hewa kuingia ili watumiaji wapate kupumua vyema.
FAIDA ZA KIAFYA ZA SAUNA:
1.Matumizi ya sauna huweza kutuliza dalili za mwili kujisikia baridi.
2.Pia kupunguza hamu ya kula na hivyo kupunguza uzito wa mwili.
3.Hupunguza uchovu wa mwili.
4.Pia hupendekezwa kutumiwa kwaajili ya kurudisha nguvu baada ya mzazi kujifungua.
5.Hupunguza / huondoa msongo wa mawazo.
6.Husafisha ngozi
7.Huleta usingizi mzito
8.Hupoza misuli na kupunguza maumivu kwenye maungio
MADHARA YA MATUMIZI YA SAUNA:
1.Watu wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo au walevi na wateja wa madawa ya kulevya huwa hatarini wakitumia sauna.
2.Matumizi ya Sauna yamethibitika kupelekea upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.Kumekuwa na ushahidi kuwa joto limekuwa na athari katika uzalishaji wa mbegu za kiume.
USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
0 COMMENTS
Chapisha Maoni