+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumatano, 29 Julai 2015

PICHA NA HISTORIA YA MAPANGO YA KONDOA IRANGI (TANZANIA)



Habari za wakati mpendwa msomaji!
Kuna sababu mbalimbali zilizopelekea binadamu kubadilisha mifumo ya kuishi (life style) na hii imesababisha mabadiliko makubwa sana katika upande wa ujenzi tokea kuishi kwenye vichaka na miamba/mapango mpaka sasa kwenye majengo. Hivyo basi hatuna budi kukupa historia za tamaduni zetu na maeneo waliyoishi miaka hiyo na kama ukivutiwa zaidi unaweza tembelea (utalii wa ndani).
Historia ya mapango ya kondoa irangi
Mapango ya kondoa irangi yapo wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania. Yapo umbali wa kilomita tisa (9) kutoka barabara kubwa inayoelekea Arusha. Mapango haya yana michoro iliyochorwa yapata miaka 1500s iliyopita na watu wa zamani, michoro hii inaonesha umbo la binadamu akiwa anawinda, anavuka mto, akipiga kifaa cha muziki na maumbo ya wanyama ambao ni tembo, twiga na paa(palahala).
Chanzo : Ukarimu blog
Picha zingine za mapango ya kondoa irangi





Kupata historia zingine bonyeza baandishi ya blue hapo chini

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zinazohusu ujenzi
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumanne, 28 Julai 2015

KAMA WEWE NI FUNDI AU DALALI WA MAMBO YA UJENZI INGIA HAPA



Habari za wakati! Nia na madhumuni ya ujumbe huu ni kukujulisha wewe dalali na fundi wa mambo ya ujenzi kama vile fundi mwashi, umeme, gypsum, rangi, bati, nk. kwamba tunataka kuwasiliana na wewe kwa ajili ya mambo mbalimbali ya kibiashara na kupeana fursa.
Unachotakiwa kufanya
Tutumie ujumbe kwenye email hii ujenzielekezi04@gmail.com au kwenye namba yetu ya simu +255 753 066 151 taarifa zifuatazo;
  • Anza na neno ujenzielekezi
  • Jina lako kamili mfano juhudi maendeleo
  • Aina ya ufundi mfano fundi rangi, kwa wale madalali andika dalali
  • Mkoa ulipo mfano Pwani
Baada ya kututumia taarifa hizo tutakutafuta kwa njia uliyotumia hapo juu (njia ya ujumbe) ndani ya masaa yasiozidi matano.
Zingatia : fata maelekezo yaliyotajwa hapo juu nasi tutakutafuta.
Mjulishe na mwingine ujumbe huu

bonyeza hayo maandishi ya blue kama wewe ni architect/msanifu majengo

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zinazohusu ujenzi
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumamosi, 25 Julai 2015

LIFAHAMU BAFU MVUKE (SAUNA)

Karibu sana mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi. Leo tunaendelea na mfululizo wa makala zetu za ujenzi kama ilivyoada.Leo tunaangazia kuhusu Sauna au Bafu mvuke. Huenda ulishawahi kusikia kuhusu hili neno au kupata kutumia kabisa chumba hiki.Sauna huweza kujengwa nje ya jengo kuu au likawa ndani ya jengo kuu.

Sauna au ( Bafu la mvuke kwa Kiswahili ) ni Chumba kidogo au jengo lililosanifiwa / buniwa kama sehemu ya kupata joto la mvuke. Mvuke ambao huweza kuwa mkavu au wenye maji maji.

Ambapo mvuke na joto la hali ya juu huwafanya watu kutoka jasho.

Leave a Reply Cancel replyWhat is the advantage of the FIR sauna over a conventional sauna _

Sauna huweza kugawanyika katika Makundi mawili.

1.BAFU MVUKE LA KAWAIDA / ASILI :

Hii ni sauna ambayo huipa hewa joto na kisha hewa kusambaa katika chumba na kuipasha ngozi.Sauna hii hupitisha joto kwa njia ya uoevu (convection).

Saunas – Types and Benefits(1)The Benefits of Sauna in Detoxification Program

2.BAFU MVUKE LA  MIALI:

Hii ni sauna ambayo hupasha vitu joto moja kwa moja.

Bafu mvuke  la miali hutumia nyenzo mbali mbali kwa ajili ya kupasha joto kama vile mkaa, nyuzi nyuzi hai za kaboni na nyenzo nyingine nyingi.

C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_640px-Geysirhöhle

infrared sauna light chromo therapy sauna aromatic bath kelo sauna

UTENDAJI KAZI WA SAUNA:

Jotoridi ambalo hukaribia 100oc (212o F) Litakuwa moja kwa moja halivumiliki kabisa.

Sauna huwekewa madirisha madogo kiasi yenye matundu ambayo huruhusu hewa kuingia ili watumiaji wapate kupumua vyema.

Openbaar saunabedrijf [ bewerken ]

FAIDA ZA KIAFYA ZA SAUNA:

1.Matumizi ya sauna huweza kutuliza dalili za mwili kujisikia baridi.

2.Pia kupunguza hamu ya kula na hivyo kupunguza uzito wa mwili.

3.Hupunguza uchovu wa mwili.

4.Pia hupendekezwa kutumiwa kwaajili ya kurudisha nguvu baada ya mzazi kujifungua.

5.Hupunguza / huondoa msongo wa mawazo.

6.Husafisha ngozi

7.Huleta usingizi mzito

8.Hupoza misuli na kupunguza maumivu kwenye maungio

MADHARA YA MATUMIZI YA SAUNA:

1.Watu wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo au walevi na wateja wa madawa ya kulevya huwa hatarini wakitumia sauna.

2.Matumizi ya Sauna yamethibitika kupelekea upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.Kumekuwa na ushahidi kuwa joto limekuwa na athari katika uzalishaji wa mbegu za kiume.

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

 

PICHA NA VITU VYA MSINGI KUWEPO KWENYE CHUMBA CHA KUPIKIA (KITCHEN)



Habari za wakati mpendwa msomaji! Karibu tena kwenye uwanja huru wa kujipatia taarifa na elimu mbadala kwa mambo ya ujenzi.

Mpendwa msomaji utaratibu wa kuweka chumba cha kupikia (kitchen) kwenye nyumba ya kuishi(residential) ulianza kuzingatiwa zaidi miaka ya 1920s na katika nchi zetu za kiafrika miaka ya 1970s japo mpaka sasa bado kuna baadhi ya maeneo haujazingatiwa. Utaratibu huu ulianzishwa hasa maeneo ya mijini kwa lengo la kupunguza matumizi ya eneo yasiyokuwa ya lazima na kwa ajili ya ulinzi(security and privacy).


Chumba cha kupikia(kitchen) ni chumba chenye pilika pilika (movement) nyingi karibia robo tatu siku (imekadiriwa kwamba mtu anayeandaa chakula kwenye chumba kisicho na mpangilio mzuri movement anazofanya ni sawa na mtu aliyetembea maili moja na nusu), hivyo basi ni vizuri kuweka mpangilio mzuri ili kupunguza pilika pilika(movement) zisizokuwa na msingi.

Kumbuka : wapo wataalamu waliobobea kwenye mambo ya upangiliaji wa ndani ya nyumba (interior designer) hivyo basi kama itakusumbua ni vizuri kumtafuta mtaalamu husika akusaidie
Vitu vya msingi kuwepo kwenye chumba cha kupikia (kitchen)
Ili twende sawa kwenye hiki chumba kuna maeneo matatu (3) ya msingi kuzingatiwa. Mwisho utaona picha kwa vielelezo.
1. sehemu ya kuhifadhi(preservation & storage) – Eneo hili ni vizuri kuwa karibu na mlango wakutokea ili iwe rahisi mtu akiingia tu anaweka vitu, katika nyumba kubwa hili eneo pia hutafutiwa chumba chake. Hapa kuna vitu vifuatavyo
  • Jokofu (refrigerator)
  • makabati (shelves or cupboard)
2. Sehemu ya maandalizi na usafishaji(preparation & cleaning) – Hapa ndiyo maandalizi ya vifaa vya kupikia pamoja na malighafi za mapishi zinapoandaliwa, ni vizuri kuwa karibu na dirisha. Vitu vinavyotakiwa kuwepo;
  • Meza (table)
  • Sink
3. Sehemu ya kupikia (cooking center) – hii ndiyo sehemu ya kutayarishia chakula, vitu vinavyotakiwa kuwepo;
  • jiko la kupikia (stove or range)
  • kabati la juu (shelves)
Picha za vielelezo


USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatano, 22 Julai 2015

angalia hapa jinsi matairi mabovu ya magari yanavyotumika kama urembo kwenye jengo



Habari za wakati mpendwa msomaji! inawezekana vitu hivi ukawa ushawahi kuviona lakini jinsi umaliziaji wake ulivyokuwa ukiambiwa ni matairi usiamini.
sasa hapa tuangalie baadhi ya picha zinazoonesha urembo katika majengo uliotumia matairi mabovu ya magari kama malighafi.
kuona urembo mwingine unaovutia uliotengenezwa kwa kutumia tairi bovu bonyeza maandishi ya blue hapo chini




UREMBO UNAOVUTIA ULIOTENGENEZWA KWA TAIRI 

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumamosi, 18 Julai 2015

JIONEE PICHA ZA NYUMBA WANAYOISHI JAY Z NA BEYONCE



Habari za wakati mpendwa msomaji! karibu tena katika blog hii inayokupatia taarifa mbalimbali na kukuelimisha katika mambo ya ujenzi.
Wakati mwingine watu hawapendi kukaa nyumbani kwa sababu kuna vitu havipo nyumbani mfano mtu ni mwanamichezo na kwake hata sehemu ya kuruka kamba haipo Je atapata vipi hamu ya kukaa nyumbani? hivyo basi ni vizuri ukiwa unafikiria kujenga nyumba ya kuishi kuangalia na mahitaji ya nafasi yako katika jamii mbali na yale tuliyozoea kama vile vyumba vya kula.
Hapa tumekuandalia picha zinazoonesha baadhi ya maeneo ya nyumba wanayokaa wasanii wakubwa duniani yaani Jay Z na Beyonce yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 43 kwa lengo la kukuonesha ni vitu/sehemu gani ambazo wao walizipa kipaumbele kuzipendezesha ili kufanya mazingira yawe rafiki na sifa zao.
Sifa za nyumba hiyo kwa picha
  • sehemu ya mbele (front)

  • sehemu ya nyuma

  • ina vyumba vya kulala 12

chumba cha kulala (self contained)

chumba cha wageni (guest room)
  • maktaba

maktaba(library)
  • chumba cha faragha (closet) cha aina yake

closet
  • chumba cha kucheza mchezo wa kitufe (bowling)

bowling
  • sehemu ya kucheza tennis

  • chumba cha habari (media room)

media room
  • chumba cha tv (tv room)

  • chumba cha michezo

skateboarding ramp
  • chumba cha mazoezi (gym)

  • bafu la mvuke (sauna)

  • sehemu ya kuogelea (pool)

Chanzo : HOME BUNCH
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Ijumaa, 17 Julai 2015

JIFUNZE HAPA KWA PICHA JINSI UNAVYOWEZA KUPENDEZESHA MAZINGIRA YA JENGO LAKO



Habari za wakati mpendwa msomaji! hapana shaka ushawahi kusikia usemi wa wahenga usemao “kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza” na ule usemao “usione vyaelea ujue vimeundwa” basi yanaakisi utakayoenda kuyaona hapa.
Kwanza kabisa utengenezaji mzuri wa mpangilio wa mazingira yanayokuzunguka husaidia vitu vingi kama kuua wadudu wanaokaa sehemu zenye uchafu, kurahisisha upitaji, kuboresha afya, na pia ni urembo.
Mbali na sifa za kutengeneza mazingira hapo juu pia kama utaweza kutengeneza vizuri inaweza kuwa fursa ya ajira maana si kila mtu anaeweza wengine huomba kusaidiwa. Pia zipo hadi kampuni zinazotoa huduma hii.
MAELEZO KWA PICHA
hatua ya kwanza

hatua ya pili

hatua ya tatu

zao lake (end product)

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Alhamisi, 16 Julai 2015

MAMBO MAWILI(2) MUHIMU ILI KUPEWA KIBALI CHA KUJENGA JENGO



Habari za wakati mpendwa msomaji! hivi kwa kawaida ni watu wangapi ambao wanafikiria kujenga? hapana shaka ukifanya utafiti utakuta kila binadamu mwenye akili timamu anafikiria kujenga. Hivyo basi twende pamoja katika habari hii muhimu kwako.
Kabla ya yote bonyeza maandishi ya bluu hapo chini ili kusoma habari zilizokwisha wekwa ambazo zinaweza kukusaidia
vitu vya kuchunguza kabla hujanunua kiwanja
Kabla hujafikiria kujenga zingatia haya
Vitu 11 vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali
Hatua za kufuata ili kupewa kibali cha kujenga jengo.
   Kwanza kabisa wanaotoa kibali cha kuruhusu jengo lijengwe  ni mamlaka za kiserikali za eneo husika hasa manispaa, kwa maana wao wanao ramani ya mji mzima inayoonesha mipangilio ya aina za majengo yanayotakiwa kujengwa katika kila mtaa.
1. Hati halali ya eneo – Hii hasa kwa wale wanaotaka kujenga majengo ya gholofa na ya kibiashara ni lazima kuhakikisha unakuwa na hati halali inayoonesha kwamba sehemu unayotaka kujenga ni mali yako.

mfano wa hati ya kiwanja
2. Michoro kamili na iliyowekwa muhuri – hii ni ile ya msanifu majengo(architectural drawings) kwa majengo ya kawaida ya kuishi(residential) ya chini (one storey) kwa yale ya ghorofa pia itahitajika michoro ya mhandisi majengo(structural drawings), mhandisi umeme (electrical drawings), na michoro ya mfumo wa maji safi na taka (plumbing).

mfano wa ramani ya muonekano wa jengo (3dimension)

 
Kumbuka : michoro hii yote inatakiwa iwe imepigwa muhuri ili kuonesha kwamba imechorwa na wataalamu wenye sifa na wanaotambulika.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
usiache kuweka neno hapo chini

Jumatano, 15 Julai 2015

SABABU ZA KUZINGATIA UKIWA UNACHAGUA VIGAE vya kusakafia KWA UJENZI WA JENGO LAKO

2

Habari za wakati mpedwa msomaji! yaweza kuwa mpaka sasa unajiuliza ni vigae gani unataka kutumia kwenye sehemu/vyumba vya jengo lako mfano sebuleni, jikoni, vyumba vya kulala, stoo, chooni, bafuni, nk. Basi majibu yake yapo hapo chini.

Aina za vigae

Kuna aina mbili za vigae

1. kutokana na malighafi/material iliyotengeneza mfano ceramic, marble, slate, porcelain, granite,carpet , nk.

3

picha ya vigae vya ceramic

2. kutokana na umbile (texture) – hapa kuna aina mbili vinavyokwaruza(grazed) na visivyokwaruza (ungrazed)

header_floor_tile

picha ya vigae vinavyokwaruza (grazed)

Sababu za kufuata ukiwa unachagua vigae vya kusakafia

1. Matumizi ya eneo husika – Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala

2. Upatikanaji – kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine iliyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.

3. Uwezo wake na muda wa kuaribika – vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.

4. Gharama (mfuko wako) – ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.

Zingatia: sababu hizi ni za msingi(basic) kwa yule anayehitaji vigae. kwa msaada zaidi onana na wataalamu husika kama wasanifu majengo(architect) au wakadiliaji ujenzi (quantity surveyor)

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506