Jumatano, 12 Agosti 2015
Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia wataalamu mbalimbali wa ujenzi wamekuwa wakifanya vitu tofauti tofauti ili kupendezesha zaidi, kurahisisha na kupunguza gharama za ujenzi.
Hapa tumekuwekea picha zinazoonesha maua ya urembo maalumu yaliyobandikwa kwa kutumia roller kwenye karatasi za ukuta (wallpaper) na mbao.
Jumamosi, 1 Agosti 2015
Katika ujenzi wa jengo kuna hatua mbalimbali mpaka jengo kukamilika. Hapa tuguse upande wa umaliziaji wa ndani (interior finishing) katika majengo ya kuishi (residential house).
Jumatano, 22 Julai 2015
sasa hapa tuangalie baadhi ya picha zinazoonesha urembo katika majengo uliotumia matairi mabovu ya magari kama malighafi.
UREMBO UNAOVUTIA ULIOTENGENEZWA KWA TAIRI
Jumatano, 15 Julai 2015
Habari za wakati mpedwa msomaji! yaweza kuwa mpaka sasa unajiuliza ni vigae gani unataka kutumia kwenye sehemu/vyumba vya jengo lako mfano sebuleni, jikoni, vyumba vya kulala, stoo, chooni, bafuni, nk. Basi majibu yake yapo hapo chini.
Aina za vigae
Kuna aina mbili za vigae
1. kutokana na malighafi/material iliyotengeneza mfano ceramic, marble, slate, porcelain, granite,carpet , nk.
picha ya vigae vya ceramic
2. kutokana na umbile (texture) – hapa kuna aina mbili vinavyokwaruza(grazed) na visivyokwaruza (ungrazed)
picha ya vigae vinavyokwaruza (grazed)
Sababu za kufuata ukiwa unachagua vigae vya kusakafia
1. Matumizi ya eneo husika – Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala
2. Upatikanaji – kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine iliyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.
3. Uwezo wake na muda wa kuaribika – vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.
4. Gharama (mfuko wako) – ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.
Zingatia: sababu hizi ni za msingi(basic) kwa yule anayehitaji vigae. kwa msaada zaidi onana na wataalamu husika kama wasanifu majengo(architect) au wakadiliaji ujenzi (quantity surveyor)
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Jumamosi, 9 Mei 2015
Kabla hujaanza ujenzi ni vyema ukabaini ni aina gani ya bati utaezeka kwenye nyumba yako.
Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kuamua aina ya ezekeo ulitalo kwenye nyumba yako:
1. Gharama ya aina ya Ezeko/Roof husika
2. Upatikanaji wake
3. Uimara wake / durability
4. Hali ya hewa i.e Uwezo wake kuhimili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ya mahali husika.
5. Mvuto / Aesthetics.
6. Salama kwa afya.
7. Rafiki wa mazingira
AINA ZA ROOFING MATERIALS AMBAZO ZINATUMIKA SANA SIKU HIZI
1. Roof Tiles (Ezeko la Vigae)
Mara nyingi hivi vigae hutengenezwa kwa udongo / clay tiles au zege /concrete tiles.
Ikumbukwe vigae vya udongo vilianza kutumika zamani sana kabla ya concrete tiles na hudumu kwa takribani miaka 50 hadi 100. Ila mbao zilizoshikilia vigae / battens & underlayments hudumu kwa takribani miaka 5-15 pekee.
2. Metal Sheets
Hizi ni paa ambazo hutengenezwa kwa metali katika viwanda kwa kupitia michakato mbalimbali ambayo mwishowe huzalisha bati nyembamba na nyoofu kabisa ambazo huwekwa katika maumbo na aina tofauti tofauti ili kukidhi uhitaji wa wanunuzi.
Faida ya kutumia metal sheets ni pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili hali mbaya ya hewa na kutoa ulinzi mathubuti kwa jengo lako. Metal Sheets
huweza kudumu hadi kwa miaka 50 ila itabidi uangalie fasteners kwa kila baada ya miaka 2 ili uweze kubaini kama zinahitajika kubadilishwa au la. Hii ni muhimu katika kuboresha umadhubuti wa utendaji kazi wa paa lako.
MATERIALS:
- Stainless steel
- Aluminium
![]() |
| metal sheets |
Jumatatu, 13 Aprili 2015
Mpendwa msomaji wa makala zetu tunaomba radhi kwa kuwa kimya kipindi kirefu kutokana na majukumu ya hapa na pale, na kwasasa tumejipanga vizuri kukuhabarisha na kukuelimisha kuhusu ujenzi karibu sana na karibu tena.
Nyavu (wire mesh) ni moja ya malighafi zinazotumika kwenye ujenzi wa majengo mbalimbali kama nyumba ya kuishi (milangoni na madirishani), na nyumba za wanyama/ndege wanaofugwa kama vile kuku, bata, kanga, N.K . Nyavu zipo za aina nyingi kulingana na ukubwa wa matundu yake
Upatikanaji
Nyavu hupatikana kwenye maduka yanayouza vifaa vya ujenzi, pia unaweza kukuta hata kwenye maduka ya vitu vigumu (hardware).
Ubora
Nyavu hutofautiana ubora kulingana na sehemu/kampuni iliyotengenezwa hivyo basi ni vizuri kununua nyavu ambazo mfuko wake unalebo na kwenye maduka yanayotambulika (usisahau risiti). Ni vizuri zaidi kutumia nyavu zilizopakwa rangi kwa ubora zaidi
Uwekaji na utunzaji
Nyavu ni kitu kinachoathirika sana na kutu hivyo basi hazitakiwi kuwekwa chini(kwenye sakafu) au sehemu yenye unyevu unyevu mfano nje ya nyumba.
Gharama yake kwa sasa
| Jina | Gharama (Tsh)/= |
| nyavu ngogo(za mbu) | 3000-4500 kipande(piece) |
| zinazofatia kwa ukubwa | 5000-7000 kipande(piece) |
kumbuka:gharama zinabadilika kutokana na eneo husika, hizi ni gharama kwa Dodoma mjini.
kwa maelezo zaidi au ushauri tuandikie kupitia email yetu ujenzielekezi04@gmail.com au piga simu namba +255653506193





















