Jumatano, 15 Julai 2015
SABABU ZA KUZINGATIA UKIWA UNACHAGUA VIGAE vya kusakafia KWA UJENZI WA JENGO LAKO
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati mpedwa msomaji! yaweza kuwa mpaka sasa unajiuliza ni vigae gani unataka kutumia kwenye sehemu/vyumba vya jengo lako mfano sebuleni, jikoni, vyumba vya kulala, stoo, chooni, bafuni, nk. Basi majibu yake yapo hapo chini.
Aina za vigae
Kuna aina mbili za vigae
1. kutokana na malighafi/material iliyotengeneza mfano ceramic, marble, slate, porcelain, granite,carpet , nk.
picha ya vigae vya ceramic
2. kutokana na umbile (texture) – hapa kuna aina mbili vinavyokwaruza(grazed) na visivyokwaruza (ungrazed)
picha ya vigae vinavyokwaruza (grazed)
Sababu za kufuata ukiwa unachagua vigae vya kusakafia
1. Matumizi ya eneo husika – Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala
2. Upatikanaji – kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine iliyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.
3. Uwezo wake na muda wa kuaribika – vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.
4. Gharama (mfuko wako) – ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.
Zingatia: sababu hizi ni za msingi(basic) kwa yule anayehitaji vigae. kwa msaada zaidi onana na wataalamu husika kama wasanifu majengo(architect) au wakadiliaji ujenzi (quantity surveyor)
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
0 COMMENTS
Chapisha Maoni