+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HISTORIA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HISTORIA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 21 Agosti 2015

HUU NDIYO MWANZO WA BINADAMU KUISHI KWENYE MAJENGO



Habari za wakati ! pasi na shaka u mzima wa afya, na kama haupo vizuri basi mungu atakujaalia kwa njia atakayopendelea maana mungu hamtupi mja wake.
Kama haujawahi kufatilia historia za mwanzo wa binadamu kuishi kwenye majengo ipo hivi;
Katika miaka ya 3500BC – 324BC (yaani kabla ya kuzaliwa yesu) watu walioanza mfumo wa kujenga walikuwa Wamisri na walikuwa wakijenga kwa madhumuni ya kuhifadhi mwili wa mfalme (FARAO) pale atakapo fariki dunia.
Mtu aliyebuni wazo hili kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri mkuu na aliitwa IMHOTEP. Cheo cha uwaziri mkuu alipewa na FARAO kwa sababu ya uwezo wake wa kujua mambo mengi kama vile uchongaji, kujenga, kutibu na kuongoza.
Muhimu : kujua zaidi historia ya imhotep endelea kutembelea mtandao huu.
Picha zingine
1. Pyramid

2. Great sphinx
3. Hekalu (temple) ya Horus

4. Hekalu la abu simbel

5. picha ya pyramid kwa ndani

Bonyeza maandishi ya blue hapo chini kupata historia nyingine kuhusu ujenzi


USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
 
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatano, 29 Julai 2015

PICHA NA HISTORIA YA MAPANGO YA KONDOA IRANGI (TANZANIA)



Habari za wakati mpendwa msomaji!
Kuna sababu mbalimbali zilizopelekea binadamu kubadilisha mifumo ya kuishi (life style) na hii imesababisha mabadiliko makubwa sana katika upande wa ujenzi tokea kuishi kwenye vichaka na miamba/mapango mpaka sasa kwenye majengo. Hivyo basi hatuna budi kukupa historia za tamaduni zetu na maeneo waliyoishi miaka hiyo na kama ukivutiwa zaidi unaweza tembelea (utalii wa ndani).
Historia ya mapango ya kondoa irangi
Mapango ya kondoa irangi yapo wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania. Yapo umbali wa kilomita tisa (9) kutoka barabara kubwa inayoelekea Arusha. Mapango haya yana michoro iliyochorwa yapata miaka 1500s iliyopita na watu wa zamani, michoro hii inaonesha umbo la binadamu akiwa anawinda, anavuka mto, akipiga kifaa cha muziki na maumbo ya wanyama ambao ni tembo, twiga na paa(palahala).
Chanzo : Ukarimu blog
Picha zingine za mapango ya kondoa irangi





Kupata historia zingine bonyeza baandishi ya blue hapo chini

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zinazohusu ujenzi
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatatu, 13 Julai 2015

HISTORIA YA LEONARDO DA VINCI KATIKA UJENZI

 

image

Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi.

katika historia leo tunamuangalia mmoja kati ya watu waliokuwa wataalamu wa kuzaliwa katika maswala ya ujenzi (msanifu majengo).

Leonardo da vinci ni msanifu majengo, mwanasayansi, mwanamuziki, mchoraji, mchongaji, mhandisi, mwanamahesabu, mwana jiolojia, mwana atonomia, na mwana botania aliyezaliwa tarehe 15 mwezi wa 4 mwaka 1452 mji wa vinci nchi ya Italy na kufariki tarehe 2 mwezi wa 5 mwaka 1519 (akiwa na miaka 67) mji wa amboise nchi ya Ufaransa

Japo ni muda wa miaka 496 umepita sasa lakini bado kazi zake zimekuwa zikitumiwa na wanasayansi katika tafiti zao, pamoja na baadhi ya picha alizozitengeneza na kuuzwa kwa gharama kama ile ya mona lisa aliyoichora mnamo mwaka 1503-1505.

image

Katika teknolojia ya ujenzi leonardo da vinci alitumia muda wake kusoma uwiano wa mwili wa binadamu (human proportional) na kuchora mchoro unaoonesha uwiano huo mnamo mwaka 1492 ambayo inatumiwa na wasanifu majengo wanapokuwa wanaanza kubuni ukubwa wa jengo.

image

 Pia katika teknolojia ya ujenzi leonardo da vinci kupitia kazi zake pamoja na maelezo yake aliyokuwa akiyaandika kwa siri (yaani mpaka uweke kioo ndiyo yanasomeka), alichora picha kuonesha muonekano wa jengo kwa kutumia uwiano wa macho (3 dimension) mnamo mwaka 1490s ambazo zinatumiwa na wasanifu majengo mpaka sasa

image

Kazi nyingine alizozifanya leonardo da vinci

Taswira ya mwanamuziki mwaka 1490

image

Taswira ya madonna na mtoto mwaka 1470s

image

Taswira ya mwili wa mwanamke mwaka 1506-08

image

Taswira ya fuvu mwaka 1489

image

Mchoro wa mashine mwaka 1480

image

Mchoro wa mashine ya kupaa (flying machine) mwaka 1486-90

image

Na hii ni kazi iliyombebea umaarufu zaidi inaitwa “the last supper” mwaka 1495-98

image

SOURCE: LEONARDO DA VINCI FOR KIDS BOOK

Ni kazi nyingi alizozifanya Leonardo da vinci ila tunaishia hapo kwa sasa, kwa historia zake zingine na za wataalamu wengine wa zamani endelea kututembelea.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumanne, 19 Mei 2015

LIFAHAMU JENGO LA KIHISTORIA LA TAJ MAHAL


--------------------------------------------------------------------------------



     Miongoni mwa vivutio vikubwa ulimwenguni ni jengo la kitamaduni la Taj Mahal.
Ambalo hupata kutembelewa na watalii takribani milioni 3 kila mwaka.
Lipo Agra nchini India lina urefu upatao m 73 (ft 240).
    Kitu kikubwa kiwavutiacho watu ni historia ya jengo hili na kisa cha ujenzi wake ukiachilia mbali ubora wa nyenzo / materials zilizo tumika kwenye ujenzi huu kwani ni jengo la muda mrefu lakini bado lipo kwenye wakatiwa  kisasa na linavutia machoni mwa watu.



Aina ya Mtindo wa kisanifu uliotumika ni Mughal Architecture
Inaaminika kuwa Taj Mahal ( hutafsiriwa kama Taji la Himaya ) ni ufupisho wa jina la Mumtaz Mahal (Aliyefahamika zaidi kama Arjumand Bano Begum).
     Ujenzi huu ambao ulitumia zaidi nyenzo za marble nyeupe , uligharamiwa na mfalme Shah Jahan (1628-1658) ambaye alijenga jengo hili ili kuenzi fikra za mke wake kipenzi miongoni mwa wake zake watatu , Mumtaz Mahal (aliyefariki mwaka 1630 AD alipokuwa akijifungua mtoto wao wa 14 , Gauhara Begum ) ambaye aliwahi kuwaza kujenga kaburi (tomb) kama dunia ambalo hakuwahi kuliona kabla.



 Ujenzi wa Taj Mahal ulianza mwaka 1632 AD na kumalizika mwaka 1653 AD.
Ujenzi wa jengo pekee ulikamilika mwaka 1648 ila ujenzi wa Mazingira ya nje ulikamilika 1653.
      Kwa miaka 21 watu takribani 20,000 walipata kuajiriwa kukamilisha ujenzi huu.
Ili kuweza kutoa huduma za malazi kwa waajiriwa hawa , Mji mdogo wa Taj Ganj ulianzishwa kwa ajili hiyo.
Na mbunifu wa Taj Mahal ni Ustad Ahmad Lahauri ambaye asili yake ni Pakistan.
Kuba / Dome la katikati lina urefu wa futi 240 ,sawa na mita 73.

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506