Jumanne, 19 Mei 2015
LIFAHAMU JENGO LA KIHISTORIA LA TAJ MAHAL
Je Umeipenda Hii Habari?
--------------------------------------------------------------------------------
Miongoni mwa vivutio vikubwa ulimwenguni ni jengo la kitamaduni la Taj Mahal.
Ambalo hupata kutembelewa na watalii takribani milioni 3 kila mwaka.
Lipo Agra nchini India lina urefu upatao m 73 (ft 240).
Kitu kikubwa kiwavutiacho watu ni historia ya jengo hili na kisa cha ujenzi wake ukiachilia mbali ubora wa nyenzo / materials zilizo tumika kwenye ujenzi huu kwani ni jengo la muda mrefu lakini bado lipo kwenye wakatiwa kisasa na linavutia machoni mwa watu.
Aina ya Mtindo wa kisanifu uliotumika ni Mughal Architecture
Inaaminika kuwa Taj Mahal ( hutafsiriwa kama Taji la Himaya ) ni ufupisho wa jina la Mumtaz Mahal (Aliyefahamika zaidi kama Arjumand Bano Begum).
Ujenzi huu ambao ulitumia zaidi nyenzo za marble nyeupe , uligharamiwa na mfalme Shah Jahan (1628-1658) ambaye alijenga jengo hili ili kuenzi fikra za mke wake kipenzi miongoni mwa wake zake watatu , Mumtaz Mahal (aliyefariki mwaka 1630 AD alipokuwa akijifungua mtoto wao wa 14 , Gauhara Begum ) ambaye aliwahi kuwaza kujenga kaburi (tomb) kama dunia ambalo hakuwahi kuliona kabla.
Ujenzi wa Taj Mahal ulianza mwaka 1632 AD na kumalizika mwaka 1653 AD.
Ujenzi wa jengo pekee ulikamilika mwaka 1648 ila ujenzi wa Mazingira ya nje ulikamilika 1653.
Kwa miaka 21 watu takribani 20,000 walipata kuajiriwa kukamilisha ujenzi huu.
Ili kuweza kutoa huduma za malazi kwa waajiriwa hawa , Mji mdogo wa Taj Ganj ulianzishwa kwa ajili hiyo.
Na mbunifu wa Taj Mahal ni Ustad Ahmad Lahauri ambaye asili yake ni Pakistan.
Kuba / Dome la katikati lina urefu wa futi 240 ,sawa na mita 73.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 COMMENTS
Chapisha Maoni