+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumatatu, 25 Mei 2015

hivi ndiyo vitu vinavyofanya bei ya viwanja iwe juu au chini

IMG_7433

Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa makala zetu za ujenzi tunatumaini tunakupatia taarifa nzuri zenye kukuelimisha kuhusu ujenzi, endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi juu ya mambo ya ujenzi.

Mpendwa msomaji hivi umeshawahi kujiuliza kwanini bei ya viwanja inatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine? au unakiwanja/viwanja unataka kuuza ushawahi kufikiria ni vitu gani vya kwanza kuangalia ili kutambua bei ya kiwanja/viwanja vyako? Jibu sahihi ni hili hapo chini.

Vitu vinavyoleta utofauti wa bei za viwanja kutoka sehemu moja hadi nyingine 

  1. Miundombinu – hapa tunamaanisha barabara, mifumo ya umeme, maji safi na majitaka. Hivyo basi viwanja ambavyo miundombinu hii hupatikana kiurahisi huwa vina bei ya juu ukilinganisha na viwanja ambavyo miundombinu hii haipatikani kirahisi.IMG_0025
  2. Asili(nature) ya eneo – Hapa tunamaanisha miinuko na udongo, yaani viwanja ambavyo huwa katika sehemu iliyoinuka (slope) huwa bei chini. Vile vile na viwanja ambavyo vipo kwenye udongo wa kichanga huwa bei chini.IMG_7447
  3. Huduma za kijamii – hii ndiyo iliyozoeleka na wengi kwamba viwanja ambavyo vipo karibu na huduma za kijamii mfano shule, soko, duka, barabara kuu, nk. huwa vinagharama kubwa.IMG_0022
  4. Majirani – Mara nyingi sifa hii inategemea eneo na eneo, yaani viwanja ambavyo vipo maeneo ambayo hayajatulia(uswailini) huwa bei chini mfano kwa wale wanaokaa dar-es-salaam kiwanja ambacho kipo maeneo ya masaki au mbezi beach huwa bei juu ukilinganisha na kile ambacho kipo buguruni au tandareIMG_0027
  5. Vipimo – Viwanja ambavyo vipo maeneo ambayo yamepimwa huwa bei ya juu ukilinganisha na vile ambavyo vipo maeneo ambayo hayajapimwa
  6. muonekano wa mnunuaji – japo hii sio sana lakini huzingatiwa na muuzaji, mfano bei atakayotajiwa mtu wa kawaida inaweza kuwa tofauti na atakayotajiwa mtu kama mkurugenzi, meneja wa kampuni flani.

NB. Ukiona kiwanja/viwanja vinauzwa bei ya juu na hivyo vitu hapo juu vinavyoonesha sifa ya kiwanja kuwa bei juu havijazingatiwa basi jua kwamba unapigwa

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia email hii ujenzielekezi04@gmail.com

0 COMMENTS

Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506