+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumamosi, 22 Agosti 2015

HIKI NDIO CHANZO CHA KIPINDUPINDU

Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu za ujenzi.
leo tutaangazia chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ambao umeukumba jamii yetu, Na tatizo hili limekuwa likijirudia takribani kwa kila mwaka nchini kwetu. Tukiwa kama wataalamu wa ujenzi, Tunaliangazia suala hili katika mtazamo nyeti na chanya kabisa.


SeemAndhra - mji uliopangiliwa vyema


Tunaamini huwezi na ni vigumu kupambana na tatizo usilolijua  sababu utashindwa kupata pa kuanzia, Ni dhahiri kuwa hii ni vita ya watu kwa watu na watu na tabia zao.
Ni vita ya watu kwa watu kwa sababu kuna watu ambao wanajua nini kifanyike ili madhara haya yasitokee na kuwa sehemu ya maisha yetu lakini wamekumbatia tatizo hili huku wakifumba macho.



Pili ni vita ya watu na tabia zao kwa maana ya kuwa sehemu kubwa ya jamii yetu imekuwa ikiishi katika mfumo usio rasmi kuona kuwa ni dehemu ya maisha yao kuishi hivyo.

Pengine tuangazie sababu hasa ambayo hupelekea heka heka na mfadhahiko mkubwa kwa jamii na serikali kwa ujumla mara tu kipindupindu kikiibuka.
Sababu ya ugonjwa huu ambao ni aibu kubwa kwa jamii ni uchafu ambao unatokana na kukosekana kwa mpangilio sahihi wa makazi ya watu.




Jamii na serikali kwa ujumla wake ni lazima zitambue kuwa jinsi mwanadamu anavyohitaji kutoa taka mwili vivyo hivyo  nyumba nayo hutoa taka mwili hizo.
Uwepo wa msongamano mkubwa wa makazi ya binadamu ambayo hayajapangiliwa sahihi ndipo utakuta katika mlango wa kuingilia wa nyumba ya mtu X ndio kuna mtaro wa maji taka umepita hapo.
Ni muhimu kufahamu kuwa, kuna maeneo mengi hayajapimwa na serikali na kumekuwa na ujenzi holera wa nyumba za makazi na mamlaka husika zikiwa kimya na cha kushangaza zaidi viongozi wa serikali za mitaa ndio vinara wakubwa wa kuwezesha uuzaji wa maeneo na kuruhusu ujenzi holera.
Yaani watumishi wa serikali hawana elimu tambuzi ya mazingira na athari zake lakini wamekuwa wakipewa majukumu mazito katika kusimamia masula ya kijamii ambayo hawana ujuzi nayo.













NINI KIFANYIKE ?.
Ni muda sahihi kabisa sasa kwa kila mmoja wetu kusema kuwa INATOSHA!! na kujitoa katika mfumo usio rasmi. Pale ambapo serikali inashindwa kunyoosha mkono kumbuka kuwa ni wewe ambaye utaumia na kurudi nyuma kimaendeleo.

  • Epuka ujenzi holera
  • Waone wataalamu wa ujenzi kabla hujaanza kujenga ili kuepuka gharama za kujitakia hapo baadae kama vile kutibu maradhi ya milipuko takribani kila mwaka.
  • Hakikisha unanunua kiwanja kilichopimwa na kimeidhinishwa kuwa ni kiwanja cha makazi ya binadamu.
  • Onana na msanifu majengo akupe ushauri na ramani sahihi kulingana na kiwanja chako kilivyo.

Hivyo UJENZI ELEKEZI TEAM inaihasa jamii kuwa makini na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kujiepusha na adha kama hizi za magonjwa ya milipuko n.k.
KUWA SEHEMU YA MABADILIKO UNAYOTAKA YATOKEE!!!
 KUONANA NA WATAALAMU WETU WA UJENZI (WASANIFU MAJENGO , MAFUNDI N.K) WASILIANA NASI KUPITIA +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Bonyeza hapa kuona jinsi matairi yanavyoweza kutumika kama urembo wa nyumba

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi












Ijumaa, 21 Agosti 2015

HUU NDIYO MWANZO WA BINADAMU KUISHI KWENYE MAJENGO



Habari za wakati ! pasi na shaka u mzima wa afya, na kama haupo vizuri basi mungu atakujaalia kwa njia atakayopendelea maana mungu hamtupi mja wake.
Kama haujawahi kufatilia historia za mwanzo wa binadamu kuishi kwenye majengo ipo hivi;
Katika miaka ya 3500BC – 324BC (yaani kabla ya kuzaliwa yesu) watu walioanza mfumo wa kujenga walikuwa Wamisri na walikuwa wakijenga kwa madhumuni ya kuhifadhi mwili wa mfalme (FARAO) pale atakapo fariki dunia.
Mtu aliyebuni wazo hili kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri mkuu na aliitwa IMHOTEP. Cheo cha uwaziri mkuu alipewa na FARAO kwa sababu ya uwezo wake wa kujua mambo mengi kama vile uchongaji, kujenga, kutibu na kuongoza.
Muhimu : kujua zaidi historia ya imhotep endelea kutembelea mtandao huu.
Picha zingine
1. Pyramid

2. Great sphinx
3. Hekalu (temple) ya Horus

4. Hekalu la abu simbel

5. picha ya pyramid kwa ndani

Bonyeza maandishi ya blue hapo chini kupata historia nyingine kuhusu ujenzi


USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
 
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumapili, 16 Agosti 2015

USHAURI KWA WALE WANAOTAKA KUJENGA NYUMBA KWENYE KIWANJA KILICHOPO KWENYE MUINUKO



Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi! Lengo letu ni kuhakikisha unaendelea kutembelea mtandao huu kwa kujifunza mambo mbalimbali ya ujenzi
Katika ujenzi kiwanja ni kipande cha eneo ambacho hutumika kwa kujenga majengo mbalimbali. viwanja hutofautiana  kutoka eneo moja hadi lingine kulingana na sura ya eneo husika kama vile bondeni, milimani na tambarare.
Katika viwanja vilivyopo kwenye maeneo yaliyoinuka hususani milimani ujenzi wake huwa tofauti katika msingi(foundation) tofauti na maeneo mengine.
Kuna vitu viwili vya kuzingatia kwa wale wanaotaka kujenga kwenye viwanja vilivyopo kwenye miinuko (slope).
1. Kujenga kwa ngazi(steps) – hii ni aina ya kujenga kwa kufuata usawa (level) ya vieneo vinavyounganisha eneo zima.


2. Kujenga kwa kuchimba/kujaza – hii ni aina ya ujenzi ambayo wajenzi huchimba/kujaza udongo kwa lengo la kusawazisha kisha kuendelea na ujenzi.

Muhimu: Unapofikiria kutengeneza ramani ya kujenga ni vyema kuzingatia hili kwa sababu unaweza kuwa na ramani nzuri lakini isijengeke kwenye kiwanja chako.

Kujifunza zaidi kuhusu viwanja bonyeza maandishi ya blue hapo chini



USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatano, 12 Agosti 2015

PICHA ZA MAUA YA UREMBO YANAYOPENDEZESHA UKUTA



Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi…!
Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia wataalamu mbalimbali wa ujenzi wamekuwa wakifanya vitu tofauti tofauti ili kupendezesha zaidi, kurahisisha na kupunguza gharama za ujenzi.
Hapa tumekuwekea picha zinazoonesha maua ya urembo maalumu yaliyobandikwa kwa kutumia roller kwenye karatasi za ukuta (wallpaper) na mbao.




Kujifunza vitu vingine kwa picha bonyeza maandishi ya blue hapo chini



USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatano, 5 Agosti 2015

NAMNA MBALIMBALI ZA KUPENDEZESHA DARI (CEILING) YA NYUMBA YAKO

UTANGULIZI:
Dari imekuwa ni sehemu amabayo inasahaulika sana katika ujenzi wa nyumba zetu kwa maana ya kuwa inapewa angalizo kidogo sana.
Lakini umaliziaji mzuri wa Dari huweza kuzidisha uzuri wa nyumba yako.
Dari imekuwa ikificha bomba za umeme na huduma nyingi ili kuondoa uzia kwa wakazi wa nyumba husika na kuwapa muonekano mzuri.
Ili kuweza kupata faida zote za Dari ni vyema kumpata fundi mzuri na mtaalamu mzuri au msanifu mzuri wa majengo wataoweza kusimamia kazi hiyo kwa ufanisi unaotakiwa.
Hivyo basi ni vyema tuangazie namna mbalimbali za kupendezesha au kumalizia vizuri Dari la nyumba yako.

NAMNA MBALIMBALI ZA UMALIZIAJI WA DARI:
Ni vizuri ukabaini kwanza ni nini unataka kupata au muonekano gani unataka kuupata kwa kulingana na wapi Dari lako linatarajiwa kujengwa, kwa maana ya kuwa kama ni sebuleni au vyumbani,au jikoni n.k.











USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zinazohusu ujenzi
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965



Jumamosi, 1 Agosti 2015

PICHA NA MAELEZO YA MATERIAL(MALIGHAFI) ZINAZOTUMIKA KUPENDEZESHA UKUTA KWA NDANI




Habari za wakati mpendwa msomaji! tunatumaini taarifa tunazokupatia zinakusaidia kwa namna moja ama nyinginekwa maana lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa kitovu cha taarifa mbalimbali za ujenzi. Hivyo basi usisite kututafuta kama unachochote kwa mawasiliano tunayoweka hapo chini (kila mwisho wa taarifa).
Katika ujenzi wa jengo kuna hatua mbalimbali mpaka jengo kukamilika. Hapa tuguse upande wa umaliziaji wa ndani (interior finishing) katika majengo ya kuishi (residential house).
Material(malighafi) zinazotumika kupendezesha ukuta wa ndani
Material hizi tunazozielezea hapa ni zile zinazowekwa kwenye ukuta uliopigwa lipu (plaster).
1. Rangi(paint) – Hizi ni zile mahususi(special) kwa kupaka kwenye nyumba zinapatikana maduka yanayouza zifaa vya ujenzi na rangi za nyumba. Ni material yaliyozoeleka na yanatumiwa na watu wengi karibia kila nyumba utakuta yametumika.


Kaa tayari: Hivi karibuni tutatoa taarifa  inayohusu aina za rangi.
2. Vigae (tiles) – Hivi ni vile mahususi(special) kwa ukuta, mara nyingi kwenye ukuta wa ndani vigae vinafaa kuwekwa sehemu zenye majimaji kama vile jikoni, chooni na bafuni.


Fahamu na hii kwa kubonyeza maandishi ya blue hapo chini
3. Karatasi za ukutani (wallpaper) – Haya ni material yanayotumiwa sana kwa sasa katika ujenzi wa nyumba za kisasa kwa sababu ukiachana na kupendezesha ukuta wako pia unaweza kubadilisha pale utakapohitaji kuyatoa.




USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506