Jumamosi, 1 Agosti 2015
PICHA NA MAELEZO YA MATERIAL(MALIGHAFI) ZINAZOTUMIKA KUPENDEZESHA UKUTA KWA NDANI
Je Umeipenda Hii Habari?
Katika ujenzi wa jengo kuna hatua mbalimbali mpaka jengo kukamilika. Hapa tuguse upande wa umaliziaji wa ndani (interior finishing) katika majengo ya kuishi (residential house).
Material(malighafi)
zinazotumika kupendezesha ukuta wa ndani
Material hizi tunazozielezea
hapa ni zile zinazowekwa kwenye ukuta uliopigwa lipu (plaster).
1. Rangi(paint) – Hizi ni zile
mahususi(special) kwa kupaka kwenye nyumba zinapatikana maduka yanayouza zifaa
vya ujenzi na rangi za nyumba. Ni material yaliyozoeleka na yanatumiwa na watu
wengi karibia kila nyumba utakuta yametumika.
Kaa tayari:
Hivi karibuni tutatoa taarifa inayohusu aina za rangi.
2. Vigae (tiles) – Hivi ni vile
mahususi(special) kwa ukuta, mara nyingi kwenye ukuta wa ndani vigae vinafaa
kuwekwa sehemu zenye majimaji kama vile jikoni, chooni na bafuni.
Fahamu na hii kwa
kubonyeza maandishi ya blue hapo chini
3. Karatasi za ukutani
(wallpaper) – Haya ni material yanayotumiwa sana kwa sasa katika ujenzi wa
nyumba za kisasa kwa sababu ukiachana na kupendezesha ukuta wako pia unaweza
kubadilisha pale utakapohitaji kuyatoa.
USIPITWE!!
Endelea kuwa nasi kwa taarifa
nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 COMMENTS
Chapisha Maoni