+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumamosi, 22 Agosti 2015

HIKI NDIO CHANZO CHA KIPINDUPINDU

Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu za ujenzi.
leo tutaangazia chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ambao umeukumba jamii yetu, Na tatizo hili limekuwa likijirudia takribani kwa kila mwaka nchini kwetu. Tukiwa kama wataalamu wa ujenzi, Tunaliangazia suala hili katika mtazamo nyeti na chanya kabisa.


SeemAndhra - mji uliopangiliwa vyema


Tunaamini huwezi na ni vigumu kupambana na tatizo usilolijua  sababu utashindwa kupata pa kuanzia, Ni dhahiri kuwa hii ni vita ya watu kwa watu na watu na tabia zao.
Ni vita ya watu kwa watu kwa sababu kuna watu ambao wanajua nini kifanyike ili madhara haya yasitokee na kuwa sehemu ya maisha yetu lakini wamekumbatia tatizo hili huku wakifumba macho.



Pili ni vita ya watu na tabia zao kwa maana ya kuwa sehemu kubwa ya jamii yetu imekuwa ikiishi katika mfumo usio rasmi kuona kuwa ni dehemu ya maisha yao kuishi hivyo.

Pengine tuangazie sababu hasa ambayo hupelekea heka heka na mfadhahiko mkubwa kwa jamii na serikali kwa ujumla mara tu kipindupindu kikiibuka.
Sababu ya ugonjwa huu ambao ni aibu kubwa kwa jamii ni uchafu ambao unatokana na kukosekana kwa mpangilio sahihi wa makazi ya watu.




Jamii na serikali kwa ujumla wake ni lazima zitambue kuwa jinsi mwanadamu anavyohitaji kutoa taka mwili vivyo hivyo  nyumba nayo hutoa taka mwili hizo.
Uwepo wa msongamano mkubwa wa makazi ya binadamu ambayo hayajapangiliwa sahihi ndipo utakuta katika mlango wa kuingilia wa nyumba ya mtu X ndio kuna mtaro wa maji taka umepita hapo.
Ni muhimu kufahamu kuwa, kuna maeneo mengi hayajapimwa na serikali na kumekuwa na ujenzi holera wa nyumba za makazi na mamlaka husika zikiwa kimya na cha kushangaza zaidi viongozi wa serikali za mitaa ndio vinara wakubwa wa kuwezesha uuzaji wa maeneo na kuruhusu ujenzi holera.
Yaani watumishi wa serikali hawana elimu tambuzi ya mazingira na athari zake lakini wamekuwa wakipewa majukumu mazito katika kusimamia masula ya kijamii ambayo hawana ujuzi nayo.













NINI KIFANYIKE ?.
Ni muda sahihi kabisa sasa kwa kila mmoja wetu kusema kuwa INATOSHA!! na kujitoa katika mfumo usio rasmi. Pale ambapo serikali inashindwa kunyoosha mkono kumbuka kuwa ni wewe ambaye utaumia na kurudi nyuma kimaendeleo.

  • Epuka ujenzi holera
  • Waone wataalamu wa ujenzi kabla hujaanza kujenga ili kuepuka gharama za kujitakia hapo baadae kama vile kutibu maradhi ya milipuko takribani kila mwaka.
  • Hakikisha unanunua kiwanja kilichopimwa na kimeidhinishwa kuwa ni kiwanja cha makazi ya binadamu.
  • Onana na msanifu majengo akupe ushauri na ramani sahihi kulingana na kiwanja chako kilivyo.

Hivyo UJENZI ELEKEZI TEAM inaihasa jamii kuwa makini na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kujiepusha na adha kama hizi za magonjwa ya milipuko n.k.
KUWA SEHEMU YA MABADILIKO UNAYOTAKA YATOKEE!!!
 KUONANA NA WATAALAMU WETU WA UJENZI (WASANIFU MAJENGO , MAFUNDI N.K) WASILIANA NASI KUPITIA +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Bonyeza hapa kuona jinsi matairi yanavyoweza kutumika kama urembo wa nyumba

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi












0 COMMENTS

Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506