+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumamosi, 20 Juni 2015

HATUA 10 ZA KUANZISHA BUSTANI YA NYUMBANI ( HOME GARDEN)

Habari za leo ndugu msomaji wa makala zetu za ujenzi, Tunatumai u mzima.
Kabla ya kuziangalia hizi hatua 10 za kuanzisha bustani yako nyumbani ni vyema tukaweza kujua umuhimu wa bustani ya nyumbani.
Amruth Home Garden is about a simple but innovative idea – to offer ___ Beautiful home garden
Baadhi ya umuhimu wa bustani ya nyumbani ni pamoja na:
1. Kupata hewa safi na ya asili
2. Kupata sehemu nzuri ya kupumzikia nje ya nyumba.
3. Kupendezesha muonekano wa nje wa nyumba yako.
4. Kupangilia  na kuainisha matumizi ya ardhi ya nje.
HATUA 10 ZA KUANZISHA BUSTANI YA NYUMBANI
1. WAZO:
Je itakuwa ni bustani ya maua? majani? au mboga mboga?.
Kama itakuwa ni maua je ya aina gani? aidha ni maua ya kudumu (Perennial Flowers) ambayo hustawi kwa muda mfupi lakini yanauwezo wa kustawi tena na tena kwa kila mwaka. au unafikiria maua ya muda mfupi ( annual flowers) ambayo utahitajika kuyapanda tena na tena katika mwaka mmoja lakini hustawi vizuri sana na kuipa nyumba yako muonekano mzuri.
Lakini unaweza ukaamua kupanda aina fulani ya maua kisha ukabadili kwa aina nyingine punde tu utakapo kufanya hivyo.
Home garden decoration
2.CHAGUA SEHEMU:
Maua yote na mboga mboga uhitaji takribani saa 6 za jua kamili kwa kila siku.
Hivyo tumia angalau siku moja kuchunguza jinsi jua linavyopita katika sehemu uliyoichagua kuanzisha bustani yako.
Kama sehemu yako haipati jua sana kwa siku ni vyema kuonana na mtaalamu ambaye atakushauri ni maua  ya aina gani au mbogamboga zipi zitafaa kwa eneo lako.
Ni vizuri kuchagua eneo ambalo lipo karibu na chanzo cha maji au katika sehemu ambayo unapendelea kutumia muda wako kukaa na sehemu ambayo itakuruhusu kutazama vivutio vilivyopo karibu na nyumba yako.
Modern beautiful home gardens designs ideas_

3. SAFISHA ARDHI:
Ondoa tabaka la ardhi ambalo lina uoto ambao huuhitaji katika eneo lako pendekezwa kisha safisha eneo lako vizuri.
4.BORESHA UDONGO:
Kama ardhi yako haina rutuba, ni vizuri ukaongeza thamani yake kwa kuongeza mbolea au tabaka la mchanganyiko wa nyasi zilizooza katika sehemu yako.
5. LIMA:
Ili kuweza kuruhusu maji kupenya kwa urahisi, lima sehemu ya ardhi yako pendekezwa.
Kabla ya Kulima hakikisha ardhi yako ina maji maji kiasi, Tafadhali sana usilime katika ardhi ambayo imekauka sana na wala ambayo ina maji maji sana kwa sababu kulima kwako kutapelekea kuharibu mshikano mzuri wa udongo wa eneo lako pendekezwa.
Kwa bustani ya maua ni vyema kulima mara moja tu kwa mwaka kabla ya kupanda kipindi cha majira ya kuchipua.Tunapendekeza kuonana na mtaalam kabla ya kuanza mchakato ili aweze kutambua aina ya udongo wa sehemu yako na kukupa ushauri wa kina.
6. PATA MICHE:
Unaweza kwenda sehemu zenye vituo vya bustani na kununua miche yako pia kumbuka kuhagua mimea inayoendana na hali ya hewa ya eneo ulilopo na aina ya udongo wa sehemu yako ulipo.
New home designs latest__ Modern homes garden designs ideas ___
7. PANDA MICHE:
Kuna baadhi ya miche inastawi zaidi kipindi cha joto au baridi ,hivyo ni vizuri kusoma maelezo vizuri ya mbegu au miche uliyopewa kabla ya kupanda ili uweze kubaini ni wakati upi ni muafaka kwa wewe kuanza kupanda.
8. MWAGILIA:
Miche haipaswi kukauka,mwagilia kila siku pindi angali midogo midogo hadi mizizi yake itapochipua. Baada ya hapo umwagiliaji utategemea na aina ya udongo wa eneo lako, na hali ya hewa ya eneo lako na kiasi cha mvua.
Modern Homes gardens designs pictures_(1)

9. PALILIA:
Mara kwa mara ondoa magugu ili bustani yako iweze kustawi vizuri. Kumbuka magugu yakiwa mengi yataharibu muonekano wa bustani yako na kuondoa mvuto.
10. MATUNZO:
Bustani yako tayari ipo kwenye mstari sahihi, zidisha bidii  kupalilia na kumwagilia.
Modern Homes gardens designs pictures_


kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Alhamisi, 11 Juni 2015

JINSI YA KUANZA KUCHORA KWA KUTUMIA AUTOCAD

autocad-logo

Mpendwa msomaji pole na majukumu ya kila siku katika harakati za kujenga uchumi wetu na wa nchi kwa ujumla.

Huu ni muendelezo wa mafundisho yanayohusu utumiaji wa program ya autocad, na ni matumaini yetu kuona ukituelewa kwa kile tunachokupatia.

kama hukufanikiwa kuona mafundisho yaliyopita usijali bonyeza kwenye maandishi  hapo chini

je unataka kujifunza autocad ingia hapa

jinsi ya kuandaa mazingira ya kuchorea kwenye program ya autocad

Kwa mtu yoyote anaeanza kuchora basi ni lazima ahakikishe toolbar hizi tatu za msingi zipo yaani

1. Draw toolbar – hii hutumika kwa kuchorea maumbo mbali mbali, mistari, nk.

2. Dimension toolbar – hii hutumika kwa kuonesha vipimo mbalimbali mfano kipimo cha mstari, duara, pembe, nk.

3. Modify toolbar – hii hutumika kwa kufanya marekebisho ya mistari au maumbo mbalimbali yaliyochorwa kwa draw toolbar

ili uweze kuelewa vizuri mpendwa msomaji, tumekuwekea link ya video hapo chini ambayo ukibonyeza itakupeleka moja kwa moja sehemu ambapo video ipo.Tumia fursa hii kuielewa vizuri program hii.

KUANGALIA VIDEO BONYEZA HAPA>>

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumanne, 9 Juni 2015

mambo ya msingi yanayotakiwa kuwepo kwenye hoteli

Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi, ni matumaini yetu umzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kawaida.

katika muendelezo wetu wa kukuelimisha na kukupa taarifa mbalimbali zinazohusu ujenzi basi hapa tutaangalia ni vitu gani vinavyokuwepo kwenye hoteli. Hii ni kwa ajili ya kuwapa japo a,b,c kwa wale wanaotaka kuwekeza kwenye biashara ya hoteli, na watumiaji wengine kwa ujumla.

Hoteli ni jengo la kibiashara ambalo hutumika kwa ajili ya malazi (accomodation), mara nyingi jengo hili hujengwa maeneo ya mjini(town hotel) au maeneo yenye vivutio vya kitalii (vacation hotel).

vitu/vyumba vinavyokuwepo ndani ya hoteli.

  1. Mapokezi/reception – hapa ndipo mahali  anapokuepo mtu atakaemuelekeza mteja nini cha kufanya/kufuata11
  2. Sehemu ya kusubiri huduma(waiting area)19
  3.  vyumba vya kulala(guest room) – hivi ni vyumba vya kulala na vyote huwa vinachoo na bafu (self). na vingine huwa vina sehemu ya wageni (suit)1615
  4. sehemu ya kupikia(kitchen)

1

  1. sehemu ya kulia chakula(restaurant)13
  2. sehemu ya kufulia na kuanikia nguo(laundry) inaweza kuwa sehemu ya wazi au chumba

2

  1. ukumbi/chumba cha mikutano (conference hall/room)18
  2. ukumbi wa shughuli mbalimbali (multipurpose room/hall).17
  3. stoo ya vitu (store room)
  4. sehemu ya kunywa vinywaji(counter/ bar)12
  5. sehemu ya kubadilisha fedha za kigeni(bureau DE change).

3

  1. vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi (exchanging room)
  2. chumba/sehemu ya kuweka jenereta (stand by generator) 

4

  1. sehemu ya kuegesha magari(car parking).

5

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

 

Jumamosi, 6 Juni 2015

FAHAMU JINSI NYUMBA UNAYOISHI INAVYOWEZA KUATHIRI MFUMO WAKO WA MAISHA WA KILA SIKU

Huenda ushawahi kujikuta au kuona baadhi ya watu wana tabia ya kuinamisha vichwa chini wakiwa wanapita mlangoni. Haijalishi wakiwa wamekwenda wapi , na pengine mlango ni mrefu tu kuliko wao.

Au  kuna baadhi ya watu huwa wanajikuta wakijikwaa kwenye ngazi wakiwa katika mazingira mageni na waliyozoea.

Hii ni athari ya kisaikolojia ambayo imeshatamalaki katika utaratibu wa kila siku wa maisha ya watu.Hivyo ni muhimu kuwa na makazi yanayo tii tabia zetu na mwenendo wa maisha yetu ya kila siku ili tuweze kupata kutawala mazingira yetu kwa ufanisi mkubwa.

Ni vizuri kufahamu kuwa kuna aina mbalimbali za tamaduni katika jamii yetu ambazo zinatofautiana sana au kwa ukaribu tu. Na kila mtu anapenda kuishi vile atakavyo ili awe huru na kuuridhisha moyo wake kulingana na tamaduni za kwao.

Mfano kuna baadhi ya makabila ni mwiko mume kukutana na mama mkwe wake kwenye ushoroba / corridor, Hivyo mtu huyu atahitaji kuishi kwenye nyumba ambayo haitampa wakati mgumu wa kuharibu uhusiano wake kifamilia

Ikumbukwe kuwa kila jambo hufanywa kwa sababu maalum, vivyo hivyo katika ujenzi yapasa kuzingatia mtindo wako wa maisha ndipo ujue uishi kwenye nyumba ya aina gani.

HIVI NDIVYO VITU  KWENYE NYUMBA AMBAVYO HUPELEKEA KUBADILISHA MFUMO WA MTU WA MAISHA:-

UKUBWA WA MLANGO:

Nyumba yenye milango ambayo ni mifupi sana, kiasi kwamba kufanya watumiaji wa nyumba kuinama ili wapate kupita hupelekea athari ya wakazi wake kuinamisha vichwa hata wakienda mahali kwingine.

Kumbuka kuwa urefu wa mlango hutofautiana mahali na mahali kulingana na hulka ya watu wa maeneo hayo.

Hivyo ni vyema uweze kujitambua urefu wako na kuwa na mlango ambao ni tiifu kwako.

Pia upana wa mlango kulingana na upana wa mwili wako.

Si vyema kujibana sana wakati wa kupita kama hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo.

NB: Kwa nchi kama Tanzania ambayo watu wake wengi sio warefu sana ambao wanachezea kwenye futi 5-6 ,unashauriwa kuwa na mlango wa urefu wa futi 7 bila kujumuisha kizingiti cha juu/ transom.

futi 8-8.5 pamoja na kizingiti cha juu/ transom.

AINA NA UKUBWA WA NGAZI :

Ngazi zipo za aina  mbalimbali kulingana na matumizi yake kwenye majengo husika.

Msanifu majengo anapaswa kuzingatia viwango pendekezwa kwa majengo tofauti tofauti.

Na kila hatua / step katika ngazi inapaswa kufanana ili kuzuia mtu kujikwaa kutokana na kutofautiana kwa urefu wa hatua za ngazi.

Front Steps Railing Design

UPANA WA USHOROBA / CORRIDOR :

Upana wa corridor hutofautiana mahali na mahali ila cha msingi ni vyema kubaini mtindo wako wa maisha na watu wa aina gani mnaoishi katika nyumba hiyo.

Recent Photos The Commons 20under20 Galleries World Map App Garden ___

Kuna tamaduni zinakataza jinsia ya kike kugusana na jinsia ya kiume sana sana wakiwa wa damu mbalimbali , Hivyo wembamba wa ushoroba itapelekea kuwafanya watu hawa wagusane kila mara wanapohitaji kupishana kwenye corridor.

ParkerStoneGt 0062

Hivyo mtu wa jamii hii akienda kuishi mahali ambapo watu wa hapo hawana utaratibu wa kwao, na wala ujenzi wa nyumba yao haukuzingatia ukubwa wa corridor ambao ungeruhusu watu kupishana bila kugusana, Hujikuta anabadilika na kuanza kufuata desturi za watu wengine.

Residential Corridor

VITU VINGINE NI PAMOJA NA UKUBWA WA CHUMBA ,SEBULE NK:

kwa maoni au ushauri au maswali yanayohusu ujenzi tuandikie kupitia ujenzielekezi04@gmail.com

Ijumaa, 5 Juni 2015

vitu vitatu (3) vya kuchunguza kabla ya kununua kiwanja

SAM_0884

Habari za wakati mpendwa msomaji.

Bila shaka hakuna mtu ambaye tangu amefikia umri wa kujitambua hajafikiria kununua au kumiliki kiwanja/viwanja, hivyo basi hapa tunataka kukueleza mambo matatu ya msingi kuchunguza ukitaka kununua.

Ili usipitwe na makala zetu zilizopita zinazohusu viwanja bonyeza maandishi ya bluu hapo chini.

hivi ndiyo vitu vinavyofanya bei ya viwanja iwe juu au chini

Mambo muhimu ya kuchunguza

1. Hati ya umiliki(hati ya kiwanja) – Kabla hujanunua kiwanja ni lazima kujihakikishia kwamba anayekuuzia ni mmiliki sahihi wa kiwanja unachonunua kwa kukagua hati ya umiliki.

1

Zingatia: inapotokea unataka kununua kiwanja kwa mmiliki ambaye hana hati ya umiliki wa kiwanja yaani labda eneo hilo halijapimwa, basi unapofanya manunuzi ni lazima kuambatanisha hati ya makubaliano(kati ya mmiliki na mnunuaji) yenye sahihi ya mmiliki, mnunuaji, na uongozi wa mtaa. Na baada ya kununua mmiliki mpya anaweza kufatilia hati ya umiliki (kwa gharama zake).

2. Kodi – hili ni jambo la msingi sana kuchunguza kabla hujanunua kiwanja kwa sababu siku hizi watu wanatumia hati za viwanja kukopa mikopo midogo midogo na hata mikubwa, hivyo basi ni lazima kuhakikisha kwamba kiwanja unachotaka kununua hakijawekwa rehani.

3. Sheria na matumizi ya baadae – Kila eneo lina mipango(plan) yake kutoka katika mamlaka husika. Mfano kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya majengo ya kibiashara, maghorofa, makazi, viwanda, na hata kwa ajili ya miundombinu. Hivyo basi unapotaka kununua kiwanja basi ni vyema kuchunguza katika mamlaka husika (mfano manispaa) ili kujua eneo hilo limetengwa kwa ajili ya nini kwa sababu isije ikawa unafikiria kujenga hoteli baadae kumbe hilo eneo ni la majengo ya kuishi na si kibiashara.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506