Jumamosi, 6 Juni 2015
FAHAMU JINSI NYUMBA UNAYOISHI INAVYOWEZA KUATHIRI MFUMO WAKO WA MAISHA WA KILA SIKU
Je Umeipenda Hii Habari?
Huenda ushawahi kujikuta au kuona baadhi ya watu wana tabia ya kuinamisha vichwa chini wakiwa wanapita mlangoni. Haijalishi wakiwa wamekwenda wapi , na pengine mlango ni mrefu tu kuliko wao.
Au kuna baadhi ya watu huwa wanajikuta wakijikwaa kwenye ngazi wakiwa katika mazingira mageni na waliyozoea.
Hii ni athari ya kisaikolojia ambayo imeshatamalaki katika utaratibu wa kila siku wa maisha ya watu.Hivyo ni muhimu kuwa na makazi yanayo tii tabia zetu na mwenendo wa maisha yetu ya kila siku ili tuweze kupata kutawala mazingira yetu kwa ufanisi mkubwa.
Ni vizuri kufahamu kuwa kuna aina mbalimbali za tamaduni katika jamii yetu ambazo zinatofautiana sana au kwa ukaribu tu. Na kila mtu anapenda kuishi vile atakavyo ili awe huru na kuuridhisha moyo wake kulingana na tamaduni za kwao.
Mfano kuna baadhi ya makabila ni mwiko mume kukutana na mama mkwe wake kwenye ushoroba / corridor, Hivyo mtu huyu atahitaji kuishi kwenye nyumba ambayo haitampa wakati mgumu wa kuharibu uhusiano wake kifamilia
Ikumbukwe kuwa kila jambo hufanywa kwa sababu maalum, vivyo hivyo katika ujenzi yapasa kuzingatia mtindo wako wa maisha ndipo ujue uishi kwenye nyumba ya aina gani.
HIVI NDIVYO VITU KWENYE NYUMBA AMBAVYO HUPELEKEA KUBADILISHA MFUMO WA MTU WA MAISHA:-
UKUBWA WA MLANGO:
Nyumba yenye milango ambayo ni mifupi sana, kiasi kwamba kufanya watumiaji wa nyumba kuinama ili wapate kupita hupelekea athari ya wakazi wake kuinamisha vichwa hata wakienda mahali kwingine.
Kumbuka kuwa urefu wa mlango hutofautiana mahali na mahali kulingana na hulka ya watu wa maeneo hayo.
Hivyo ni vyema uweze kujitambua urefu wako na kuwa na mlango ambao ni tiifu kwako.
Pia upana wa mlango kulingana na upana wa mwili wako.
Si vyema kujibana sana wakati wa kupita kama hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo.
NB: Kwa nchi kama Tanzania ambayo watu wake wengi sio warefu sana ambao wanachezea kwenye futi 5-6 ,unashauriwa kuwa na mlango wa urefu wa futi 7 bila kujumuisha kizingiti cha juu/ transom.
futi 8-8.5 pamoja na kizingiti cha juu/ transom.
AINA NA UKUBWA WA NGAZI :
Ngazi zipo za aina mbalimbali kulingana na matumizi yake kwenye majengo husika.
Msanifu majengo anapaswa kuzingatia viwango pendekezwa kwa majengo tofauti tofauti.
Na kila hatua / step katika ngazi inapaswa kufanana ili kuzuia mtu kujikwaa kutokana na kutofautiana kwa urefu wa hatua za ngazi.
UPANA WA USHOROBA / CORRIDOR :
Upana wa corridor hutofautiana mahali na mahali ila cha msingi ni vyema kubaini mtindo wako wa maisha na watu wa aina gani mnaoishi katika nyumba hiyo.
Kuna tamaduni zinakataza jinsia ya kike kugusana na jinsia ya kiume sana sana wakiwa wa damu mbalimbali , Hivyo wembamba wa ushoroba itapelekea kuwafanya watu hawa wagusane kila mara wanapohitaji kupishana kwenye corridor.
Hivyo mtu wa jamii hii akienda kuishi mahali ambapo watu wa hapo hawana utaratibu wa kwao, na wala ujenzi wa nyumba yao haukuzingatia ukubwa wa corridor ambao ungeruhusu watu kupishana bila kugusana, Hujikuta anabadilika na kuanza kufuata desturi za watu wengine.
VITU VINGINE NI PAMOJA NA UKUBWA WA CHUMBA ,SEBULE NK:
kwa maoni au ushauri au maswali yanayohusu ujenzi tuandikie kupitia ujenzielekezi04@gmail.com
0 COMMENTS
Chapisha Maoni