Jumatano, 13 Mei 2015
JINSI YA KUPENDEZESHA USO WA MBELE WA NYUMBA ( FRONT FACADE)
Je Umeipenda Hii Habari?
Pasi na shaka ndaniye, Kitu cha kwanza ambacho mgeni wako anapaswa kukitanabahi pindi ajapo kwako ni kuona uso wa nyumba ambao utamkaribisha kwa bashasha tele.
Hivyo kuna kila sababu ya kutumia nguvu kubwa kutengeneza uso wa mbele wa nyumba.
Kuna nyumba nyingine zimekosa muonekano mzuri wa mbele hivyo husababisha kushindwa kutofautisha uso wa mbele na uso wa nyuma wa nyumba au na upande wa kulia na kushoto.
Hivyo Msanifu wa majengo hana budi kutumia maarifa kuandaa ramani ambayo itakidhi mahitaji ya Nyumba husika.
BAADHI YA SEHEMU AMBAZO UNAWEZA KUPENDEZESHA KWENYE NYUMBA.
1. Nguzo
Hii ni moja ya sehemu ya jengo ambayo ni nyoofu. Inaweza ikawa ya umbo la duara au,mstatili au mraba kulingana na mahitaji yako.
Aina tofauti za usanifu zaweza tumiwa ili kukidhi haja ya mahitaji husika.
Mitindo itumiwayo sana kwenye nguzo ni pamoja na Doric , Ionic na Corinthian ambapo usanifu mwingine huweza kuchukua nafasi hapa.
2. Urembo Kwenye Archs
Unaweza ukaambatanisha na Keystone au Ukaacha hivi hivi na bado Arch ikawa nzuri tu.
Tumia nyenzo/ material ambazo ni rafiki wa mvuto kwa macho.
3. Madirisha
Kwakutegemea na vigezo vya sehemu au sababu za kisanifu, Msanifu ataweza kupendekeza aina ya dirisha kwa kutegemea anataraji kuweka athari kwenye nini i.e unyoofu (verticality ) au mlalo ( horizontality).
4. Milango Ya Nje
Aina mbali mbali za milango hutumiwa kwa kuzingatia aina ya mtiririko (pattern) sanifu wa msanifu ili kutokupoteza mtiririko mzima wa umoja wa mtindo wa mpangilio wa jengo ulivyochaguliwa.
5.Kuta
6. Nakshi nyingine za Kisanifu
Nakshi nyingine ni kama vile Quoin ambayo huweza kutumika kwenye kona za pembe ya nyumba.
0 COMMENTS
Chapisha Maoni