Jumatano, 20 Mei 2015
JINSI YA KUANDAA MAZINGIRA YA KUCHOREA kwenye program ya autocad
Je Umeipenda Hii Habari?
Unapofungua AutoCAD kwa mara ya kwanza kuna baadhi ya toolbar huonekana kama tulivyozielezea kwenye sehemu ya kwanza, lakini vilevile kuna ambazo zimejificha (hide) ambazo hazionekani mpaka uzitafute zilipo.
Jinsi ya kuzirudisha/kuzifungua toolbar ambazo zimejificha.
kuna njia mbili:
1. unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye sehemu iliyowazi(blank area) yaani ambayo haina toolbar yeyote, unabonyeza kitufe cha kulia(right click) cha kipanya(mouse), unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye sehemu iliyoandikwa ACAD, hapo usibonyeze itakuletea yenyewe orodha ya toolbar zote zilizokuwa zimefichwa na ambazo zinaonekana ulipofungua program
NB. Zilizowekewa alama ya pata ndizo zinazoonekana kwenye program na ambazo hazijawekewa ndiyo ambazo zimejificha kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini
2. Hii ndiyo nyepesi Zaidi, unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye ikoni yeyote iliyokwenye toolbar yeyote mfano toolbar ya kuchorea (draw toolbar) katika ikoni ya mstari (line icon), kisha unabonyeza kitufe cha kulia (right click) cha kipanya, hapo tayari itakuletea orodha ya toolbar zote ambazo zimefichwa na ambazo hazijafichwa kama invyoonekana kwenye picha hapo chini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 COMMENTS
Chapisha Maoni