Jumanne, 26 Mei 2015
zifahamu kazi na wajibu wa mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor) katika ujenzi
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati huu mpendwa msomaji, ahsante kwa kuendelea kuwa sehemu sahihi inayokupatia taarifa mbali mbali zinazohusu ujenzi. Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zaidi zinazokuja.
Mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor/ building economy) ni mtaalamu anaefuatia baada ya mtaalamu anaehusika na ubunifu na uchoraji (msanifu majengo) kumalisha kazi ya kutengeneza michoro.
http://ujenzielekezi.blogspot.com/2015/05/zifahamu-kazi-na-wajibu-wa-msanifu.html
Kazi/wajibu wa mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor)
Kwa kufuata michoro iliyochorwa kazi na wajibu wa mkadiliaji ujenzi ni;
- Kufanya makadilio ya gharama ya jengo kwanzia mwanzo hadi mwisho, kwa kuzingatia malighafi(material) yaliyopendekezwa na msanifu majengo(architect)
- Kuandaa hati ya vipimo na gharama (bills of quantity)
- kuandaa na kupitia mikataba ya uzabuni (tender documents)
- kuandaa ripoti za fedha (financial report)
- kutoa ushauri wa mambo ya gharama za ujenzi, mfano vifaa, malighafi, nk.
kwa wale wanaotaka kusomea utaalamu huu ngazi ya shahada (degree/bachelor) kwa Tanzania inatolewa ardhi university(ARU).
Na kwa wale wenye michoro wanataka kujua gharama za ujenzi, au wale wanaotaka kufanyiwa Tathmini ya gharama za majengo yao BASI hawa ndiyo dawa ya matatizo hayo.
Kufahamu wataalamu wengine wanaohusika bonyeza maandishi hayo ya bluu hapo chini
http://ujenzielekezi.blogspot.com/2014/11/hii-ndiyo-orodha-ya-watu-wanaohusika.html
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
0 COMMENTS
Chapisha Maoni