+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumapili, 3 Mei 2015

je unataka kujifunza autocad? ingia hapa.

UTANGULIZI

AutoCAD ni moja ya program au software inayotumiwa na wahandisi, wasanifu majengo, wachoraji, wapima ramani, nk. Kwa ajili ya kuchorea. Kutokana na kukua kwa utandawazi program hii imeweza kusaidia watumiaji kuondoka katika mifumo ya kuchora kwa mkono. Ukiachana na kuwepo kwa program hii kuna program nyingine nyingi ambazo hutumika kuchorea nazo ni kama Arch Cad, vector, home sweet designer, nk. Lakini zimeonekana kuwa ngumu kutumia na kuwa na vitu visivyokidhi mahitaji ya wengine.

MWANZO (SEHEMU YA KWANZA)

Unapokuwa umekwisha iweka(install) program hii kwenye computer yako ukiifungua itaonekana kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

5

 

No.

JINA

KAZI

1.

Title bar

Kuonesha jina la mchoro uliofunguliwa kutokana na jinsi ulivyotunzwa(save) mf. Document 1. Na sehemu inayofunga(close), kupunguza (restore), na kufunika mchoro(minimize/maximize)

2.

Menu bar

Kuonesha vitu vyote vinavyomsaidia mtumiaji kutumia katika program hii mf. File,view,edit, nk.

3.

Standard toolbar

Kuonesha vitufe ambavyo hutumiwa mara nyingi na mtumiaji mf. New, open, save, nk.

4.

Styles

Kuonesha aina ya maneno(text), vipimo(dimension), na table. Mara nyingi huandika standard.

5.

Workspaces

Kuonesha aina ya sehemu ya kuchorea inaweza kuwa vipimo viwili(2 dimension) au vipimo vitatu(3 dimension) mf. 3d modelling, au autocad classic

6.

Layers

Kuonesha aina ipi ya maandishi uliyoitengeneza unayoitumia.

7.

Properties

Kuonesha aina ipi ya unene/rangi uliyoitengeneza unayoitumia.

8.

Draw toolbar

Huonesha vitufe vinavyotumika kutengenezea mchoro mf. Line, rectangular, arch, nk.

9.

Modify toolbar

Huonesha vitufe vinavyotumika kufanyia marekebisho au niongeza ya vitu vilivyochorwa mf. Erase, trim, offset, nk.

10.

Dimension toolbar

Huonesha vitufe vinavyomika kupima vitu vilivyochorwa mf. Linear dimension, radius, diameter, nk.

11.

Layout

Huonesha mazingira ya kuchorea(model)/ kuchapia(print) mchoro mf. Model, layout 1, nk.

12.

Info toolbar

Huonesha maelekezo unayofuata baada ya kubonyeza kitufe chochote.

13.

Status toolbar

Huonesha maelezo ya kimahesabu yaliyopo sehemu ya kuchorea pamoja na vitufe vinavyotumika kuongeza ufanisi katika kuchora mf. Ortho, osnap, line weight type, nk.

14

Working area

Hii ndiyo sehemu ya kuchorea

NB. Pia unaweza kufungua kwa mara ya kwanza program ya autocad lakini ukakuta vitu hivi vimepungua. Jinsi ya kuvirudisha na kuona vingine fuatilia sehemu ya pili.

3 COMMENTS

Unknown alisema ...
26 Julai 2016, 03:48

nahitaji pro hii


Erdon alisema ...
14 Desemba 2017, 02:58

je ! software hii yanapatikana ktk play store au apple????


DEVOUT BUILDING CONSTRUCTION alisema ...
3 Oktoba 2019, 11:38

Ahsante kwa elimu hiyo. Barikiwa


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506