Jumapili, 3 Mei 2015
je unataka kujifunza autocad? ingia hapa.
Je Umeipenda Hii Habari?
UTANGULIZI
AutoCAD ni moja ya program au software inayotumiwa na wahandisi, wasanifu majengo, wachoraji, wapima ramani, nk. Kwa ajili ya kuchorea. Kutokana na kukua kwa utandawazi program hii imeweza kusaidia watumiaji kuondoka katika mifumo ya kuchora kwa mkono. Ukiachana na kuwepo kwa program hii kuna program nyingine nyingi ambazo hutumika kuchorea nazo ni kama Arch Cad, vector, home sweet designer, nk. Lakini zimeonekana kuwa ngumu kutumia na kuwa na vitu visivyokidhi mahitaji ya wengine.
MWANZO (SEHEMU YA KWANZA)
Unapokuwa umekwisha iweka(install) program hii kwenye computer yako ukiifungua itaonekana kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
No. | JINA | KAZI |
1. | Title bar | Kuonesha jina la mchoro uliofunguliwa kutokana na jinsi ulivyotunzwa(save) mf. Document 1. Na sehemu inayofunga(close), kupunguza (restore), na kufunika mchoro(minimize/maximize) |
2. | Menu bar | Kuonesha vitu vyote vinavyomsaidia mtumiaji kutumia katika program hii mf. File,view,edit, nk. |
3. | Standard toolbar | Kuonesha vitufe ambavyo hutumiwa mara nyingi na mtumiaji mf. New, open, save, nk. |
4. | Styles | Kuonesha aina ya maneno(text), vipimo(dimension), na table. Mara nyingi huandika standard. |
5. | Workspaces | Kuonesha aina ya sehemu ya kuchorea inaweza kuwa vipimo viwili(2 dimension) au vipimo vitatu(3 dimension) mf. 3d modelling, au autocad classic |
6. | Layers | Kuonesha aina ipi ya maandishi uliyoitengeneza unayoitumia. |
7. | Properties | Kuonesha aina ipi ya unene/rangi uliyoitengeneza unayoitumia. |
8. | Draw toolbar | Huonesha vitufe vinavyotumika kutengenezea mchoro mf. Line, rectangular, arch, nk. |
9. | Modify toolbar | Huonesha vitufe vinavyotumika kufanyia marekebisho au niongeza ya vitu vilivyochorwa mf. Erase, trim, offset, nk. |
10. | Dimension toolbar | Huonesha vitufe vinavyomika kupima vitu vilivyochorwa mf. Linear dimension, radius, diameter, nk. |
11. | Layout | Huonesha mazingira ya kuchorea(model)/ kuchapia(print) mchoro mf. Model, layout 1, nk. |
12. | Info toolbar | Huonesha maelekezo unayofuata baada ya kubonyeza kitufe chochote. |
13. | Status toolbar | Huonesha maelezo ya kimahesabu yaliyopo sehemu ya kuchorea pamoja na vitufe vinavyotumika kuongeza ufanisi katika kuchora mf. Ortho, osnap, line weight type, nk. |
14 | Working area | Hii ndiyo sehemu ya kuchorea |
NB. Pia unaweza kufungua kwa mara ya kwanza program ya autocad lakini ukakuta vitu hivi vimepungua. Jinsi ya kuvirudisha na kuona vingine fuatilia sehemu ya pili.
3 COMMENTS
26 Julai 2016, 03:48
nahitaji pro hii
14 Desemba 2017, 02:58
je ! software hii yanapatikana ktk play store au apple????
3 Oktoba 2019, 11:38
Ahsante kwa elimu hiyo. Barikiwa
Chapisha Maoni