Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo VIFAA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo VIFAA. Onyesha machapisho yote
Jumamosi, 25 Julai 2015
Habari za wakati mpendwa
msomaji! Karibu tena kwenye uwanja huru wa kujipatia taarifa na elimu mbadala
kwa mambo ya ujenzi.
Mpendwa msomaji utaratibu wa
kuweka chumba cha kupikia (kitchen) kwenye nyumba ya kuishi(residential) ulianza
kuzingatiwa zaidi miaka ya 1920s na katika nchi zetu za kiafrika miaka ya 1970s
japo mpaka sasa bado kuna baadhi ya maeneo haujazingatiwa. Utaratibu huu
ulianzishwa hasa maeneo ya mijini kwa lengo la kupunguza matumizi ya eneo
yasiyokuwa ya lazima na kwa ajili ya ulinzi(security and privacy).
Chumba cha kupikia(kitchen) ni
chumba chenye pilika pilika (movement) nyingi karibia robo tatu siku
(imekadiriwa kwamba mtu anayeandaa chakula kwenye chumba kisicho na mpangilio
mzuri movement anazofanya ni sawa na mtu aliyetembea maili moja na nusu), hivyo
basi ni vizuri kuweka mpangilio mzuri ili kupunguza pilika pilika(movement)
zisizokuwa na msingi.
Kumbuka : wapo
wataalamu waliobobea kwenye mambo ya upangiliaji wa ndani ya nyumba (interior
designer) hivyo basi kama itakusumbua ni vizuri kumtafuta mtaalamu husika
akusaidie
Vitu vya msingi
kuwepo kwenye chumba cha kupikia (kitchen)
Ili twende sawa kwenye hiki
chumba kuna maeneo matatu (3) ya msingi kuzingatiwa. Mwisho utaona picha kwa
vielelezo.
1. sehemu ya
kuhifadhi(preservation & storage) – Eneo hili ni vizuri kuwa karibu na
mlango wakutokea ili iwe rahisi mtu akiingia tu anaweka vitu, katika nyumba
kubwa hili eneo pia hutafutiwa chumba chake. Hapa kuna vitu
vifuatavyo
-
Jokofu (refrigerator)
-
makabati (shelves or cupboard)
2. Sehemu ya maandalizi na
usafishaji(preparation & cleaning) – Hapa ndiyo maandalizi ya vifaa vya
kupikia pamoja na malighafi za mapishi zinapoandaliwa, ni vizuri kuwa karibu na
dirisha. Vitu vinavyotakiwa kuwepo;
-
Meza (table)
-
Sink
3. Sehemu ya kupikia (cooking
center) – hii ndiyo sehemu ya kutayarishia chakula, vitu vinavyotakiwa
kuwepo;
-
jiko la kupikia (stove or range)
-
kabati la juu (shelves)
Picha za
vielelezo
USIPITWE!!
Endelea kuwa nasi kwa taarifa
nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Jumanne, 14 Julai 2015
Habari za wakati mpendwa msomaji! katika mada
hii tunataka tukupitishe kwenye mambo yahusuyo vifaa vya kiufundi. Hii ni kwa
ajili ya wewe fundi unaetaka kuanza shughuli(kujitegemea), au wale watu
wanaotaka kuanzisha kamradi kadogo, na pia hata kwa wale watu wanaopenda viwepo
majumbani kwao kwaajili ya mambo ya dharura au kupunguza makali ya gharama za
kiufundi.
VIFAA VYA MSINGI KWA MAFUNDI
BOMBA(PLUMBING)
1. Koleo (tongue & groove
pliers) – kazi yake ni kukaza, kulegeza na kuvuta kipande cha bomba(connector)
au nati. zipo za nchi 10 na nchi 12.
2. msumeno (hacksaw) – kazi
yake ni kukata vipande vya bomba na nati.
3. kinoleo (metal file) – kazi
yake ni kunoa (kurudisha makali) ya mabomba ya metali.
4. Basin wrench – kazi yake ni
kukaza na kulegeza nati.
5. pipe wrench – hii pia
hutumika kukazia na kulegeza nati ndogo zaidi na za ukubwa tofauti.
6. Adjustable wrench – kazi
yake ni kubana sehemu zinazohitajika kubana kama kwenye baadhi ya sehemu
zilizoungana (connector)
7. Propane torch – hili ni
dumu/kidumu kilicho na gesi, kazi yake ni kuyeyusha mabomba hasa mabomba ya kopa
sehemu za kuunganishia.
8. Hand auger – kazi yake ni
kusafisha sink, tube na mabomba.
9. Tubing cutter – kifaa hiki
kinatumika kwa kukata kwa urahisi mabomba hasa hasa mabomba ya kopa.
10. Plunger – kazi yake ni
kutoa uchafu kwenye vyoo, bafu na sink.
11. Closet auger – kazi yake ni
kusafisha sehemu za ndani za mabomba sink, vyoo nk.
12. koti gumu (overall) – kazi
yake ni kujikinga na moto, vitu vichafu na kuwa salama kiafya.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
usiache kuweka neno hapo
chini
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)














