Jumamosi, 25 Julai 2015
PICHA NA VITU VYA MSINGI KUWEPO KWENYE CHUMBA CHA KUPIKIA (KITCHEN)
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati mpendwa
msomaji! Karibu tena kwenye uwanja huru wa kujipatia taarifa na elimu mbadala
kwa mambo ya ujenzi.
Mpendwa msomaji utaratibu wa
kuweka chumba cha kupikia (kitchen) kwenye nyumba ya kuishi(residential) ulianza
kuzingatiwa zaidi miaka ya 1920s na katika nchi zetu za kiafrika miaka ya 1970s
japo mpaka sasa bado kuna baadhi ya maeneo haujazingatiwa. Utaratibu huu
ulianzishwa hasa maeneo ya mijini kwa lengo la kupunguza matumizi ya eneo
yasiyokuwa ya lazima na kwa ajili ya ulinzi(security and privacy).
Chumba cha kupikia(kitchen) ni
chumba chenye pilika pilika (movement) nyingi karibia robo tatu siku
(imekadiriwa kwamba mtu anayeandaa chakula kwenye chumba kisicho na mpangilio
mzuri movement anazofanya ni sawa na mtu aliyetembea maili moja na nusu), hivyo
basi ni vizuri kuweka mpangilio mzuri ili kupunguza pilika pilika(movement)
zisizokuwa na msingi.
Kumbuka : wapo
wataalamu waliobobea kwenye mambo ya upangiliaji wa ndani ya nyumba (interior
designer) hivyo basi kama itakusumbua ni vizuri kumtafuta mtaalamu husika
akusaidie
Vitu vya msingi
kuwepo kwenye chumba cha kupikia (kitchen)
Ili twende sawa kwenye hiki
chumba kuna maeneo matatu (3) ya msingi kuzingatiwa. Mwisho utaona picha kwa
vielelezo.
1. sehemu ya
kuhifadhi(preservation & storage) – Eneo hili ni vizuri kuwa karibu na
mlango wakutokea ili iwe rahisi mtu akiingia tu anaweka vitu, katika nyumba
kubwa hili eneo pia hutafutiwa chumba chake. Hapa kuna vitu
vifuatavyo
-
Jokofu (refrigerator)
-
makabati (shelves or cupboard)
2. Sehemu ya maandalizi na
usafishaji(preparation & cleaning) – Hapa ndiyo maandalizi ya vifaa vya
kupikia pamoja na malighafi za mapishi zinapoandaliwa, ni vizuri kuwa karibu na
dirisha. Vitu vinavyotakiwa kuwepo;
-
Meza (table)
-
Sink
3. Sehemu ya kupikia (cooking
center) – hii ndiyo sehemu ya kutayarishia chakula, vitu vinavyotakiwa
kuwepo;
-
jiko la kupikia (stove or range)
-
kabati la juu (shelves)
Picha za
vielelezo
USIPITWE!!
Endelea kuwa nasi kwa taarifa
nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
1 COMMENT
31 Agosti 2023, 03:46
Sawa nataka kujiunga nqnyi
Chapisha Maoni