Jumatatu, 13 Julai 2015
HISTORIA YA LEONARDO DA VINCI KATIKA UJENZI
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi.
katika historia leo tunamuangalia mmoja kati ya watu waliokuwa wataalamu wa kuzaliwa katika maswala ya ujenzi (msanifu majengo).
Leonardo da vinci ni msanifu majengo, mwanasayansi, mwanamuziki, mchoraji, mchongaji, mhandisi, mwanamahesabu, mwana jiolojia, mwana atonomia, na mwana botania aliyezaliwa tarehe 15 mwezi wa 4 mwaka 1452 mji wa vinci nchi ya Italy na kufariki tarehe 2 mwezi wa 5 mwaka 1519 (akiwa na miaka 67) mji wa amboise nchi ya Ufaransa
Japo ni muda wa miaka 496 umepita sasa lakini bado kazi zake zimekuwa zikitumiwa na wanasayansi katika tafiti zao, pamoja na baadhi ya picha alizozitengeneza na kuuzwa kwa gharama kama ile ya mona lisa aliyoichora mnamo mwaka 1503-1505.
Katika teknolojia ya ujenzi leonardo da vinci alitumia muda wake kusoma uwiano wa mwili wa binadamu (human proportional) na kuchora mchoro unaoonesha uwiano huo mnamo mwaka 1492 ambayo inatumiwa na wasanifu majengo wanapokuwa wanaanza kubuni ukubwa wa jengo.
Pia katika teknolojia ya ujenzi leonardo da vinci kupitia kazi zake pamoja na maelezo yake aliyokuwa akiyaandika kwa siri (yaani mpaka uweke kioo ndiyo yanasomeka), alichora picha kuonesha muonekano wa jengo kwa kutumia uwiano wa macho (3 dimension) mnamo mwaka 1490s ambazo zinatumiwa na wasanifu majengo mpaka sasa
Kazi nyingine alizozifanya leonardo da vinci
Taswira ya mwanamuziki mwaka 1490
Taswira ya madonna na mtoto mwaka 1470s
Taswira ya mwili wa mwanamke mwaka 1506-08
Taswira ya fuvu mwaka 1489
Mchoro wa mashine mwaka 1480
Mchoro wa mashine ya kupaa (flying machine) mwaka 1486-90
Na hii ni kazi iliyombebea umaarufu zaidi inaitwa “the last supper” mwaka 1495-98
SOURCE: LEONARDO DA VINCI FOR KIDS BOOK
Ni kazi nyingi alizozifanya Leonardo da vinci ila tunaishia hapo kwa sasa, kwa historia zake zingine na za wataalamu wengine wa zamani endelea kututembelea.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
0 COMMENTS
Chapisha Maoni