+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumamosi, 9 Mei 2015

ZIFAHAMU AINA MBALIMBALI ZA ROOFING MATERIALS


Kabla hujaanza ujenzi ni vyema ukabaini ni aina gani ya bati utaezeka kwenye nyumba yako.
Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kuamua aina ya ezekeo ulitalo kwenye nyumba yako:

1. Gharama ya aina ya Ezeko/Roof husika
2. Upatikanaji wake
3. Uimara wake / durability
4. Hali ya hewa i.e Uwezo wake kuhimili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ya mahali husika.
5. Mvuto / Aesthetics.
6. Salama kwa afya.
7. Rafiki wa mazingira 

AINA ZA ROOFING MATERIALS AMBAZO ZINATUMIKA SANA SIKU HIZI

1. Roof Tiles (Ezeko la Vigae)

Mara nyingi hivi vigae hutengenezwa kwa udongo / clay tiles au zege /concrete tiles.
Ikumbukwe vigae vya udongo vilianza kutumika zamani sana kabla ya concrete tiles na hudumu kwa takribani miaka 50 hadi 100. Ila mbao zilizoshikilia vigae / battens & underlayments hudumu kwa takribani miaka 5-15 pekee.

vigae vya udongo/clay tiles

vigae vya zege jepesi/lightweight-concrete tiles


2. Metal Sheets
Hizi ni paa ambazo hutengenezwa kwa metali katika viwanda kwa kupitia michakato mbalimbali ambayo mwishowe huzalisha bati nyembamba na nyoofu kabisa ambazo huwekwa katika maumbo na aina tofauti tofauti ili kukidhi uhitaji wa wanunuzi.

Faida ya kutumia metal sheets ni pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili hali mbaya ya hewa na kutoa ulinzi mathubuti kwa jengo lako. Metal Sheets
huweza kudumu hadi kwa miaka 50 ila itabidi uangalie fasteners kwa kila baada ya miaka 2 ili uweze kubaini kama zinahitajika kubadilishwa au la. Hii ni muhimu katika kuboresha umadhubuti wa utendaji kazi wa paa lako.

MATERIALS:

  • Stainless steel
  • Aluminium
kupata kufahahamu zaidi Ubora na Gage wa stainless steel na aluminium soma hapa



metal sheets


IT 5 SHEETS




2 COMMENTS

ABRAH ONLINE alisema ...
1 Desemba 2020, 19:31

Tumeni Na ramani tuangalie


Bila jina alisema ...
26 Februari 2024, 01:43

I beloved your post. You do have a way with phrases. I felt like I was during the sauna with you. What a beautiful knowledge!   saunajournal.com


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506