Ijumaa, 5 Juni 2015
vitu vitatu (3) vya kuchunguza kabla ya kununua kiwanja
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati mpendwa msomaji.
Bila shaka hakuna mtu ambaye tangu amefikia umri wa kujitambua hajafikiria kununua au kumiliki kiwanja/viwanja, hivyo basi hapa tunataka kukueleza mambo matatu ya msingi kuchunguza ukitaka kununua.
Ili usipitwe na makala zetu zilizopita zinazohusu viwanja bonyeza maandishi ya bluu hapo chini.
hivi ndiyo vitu vinavyofanya bei ya viwanja iwe juu au chini
Mambo muhimu ya kuchunguza
1. Hati ya umiliki(hati ya kiwanja) – Kabla hujanunua kiwanja ni lazima kujihakikishia kwamba anayekuuzia ni mmiliki sahihi wa kiwanja unachonunua kwa kukagua hati ya umiliki.
Zingatia: inapotokea unataka kununua kiwanja kwa mmiliki ambaye hana hati ya umiliki wa kiwanja yaani labda eneo hilo halijapimwa, basi unapofanya manunuzi ni lazima kuambatanisha hati ya makubaliano(kati ya mmiliki na mnunuaji) yenye sahihi ya mmiliki, mnunuaji, na uongozi wa mtaa. Na baada ya kununua mmiliki mpya anaweza kufatilia hati ya umiliki (kwa gharama zake).
2. Kodi – hili ni jambo la msingi sana kuchunguza kabla hujanunua kiwanja kwa sababu siku hizi watu wanatumia hati za viwanja kukopa mikopo midogo midogo na hata mikubwa, hivyo basi ni lazima kuhakikisha kwamba kiwanja unachotaka kununua hakijawekwa rehani.
3. Sheria na matumizi ya baadae – Kila eneo lina mipango(plan) yake kutoka katika mamlaka husika. Mfano kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya majengo ya kibiashara, maghorofa, makazi, viwanda, na hata kwa ajili ya miundombinu. Hivyo basi unapotaka kununua kiwanja basi ni vyema kuchunguza katika mamlaka husika (mfano manispaa) ili kujua eneo hilo limetengwa kwa ajili ya nini kwa sababu isije ikawa unafikiria kujenga hoteli baadae kumbe hilo eneo ni la majengo ya kuishi na si kibiashara.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
0 COMMENTS
Chapisha Maoni