+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumamosi, 23 Mei 2015

KABLA HUJAFIKIRIA KUJENGA ZINGATIA HAYA

Kwa kawaida ukifikiria kujenga huwa huwazi juu ya hali ya hewa na wala hufikirii kuhusu nyenzo / materials za ujenzi kama zitakuwa kikwazo katika ujenzi wako.

Katika tovuti hii tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali za ujenzi ili kukufumbua macho zaidi na kurahisisha shughuli ya ujenzi kwako.

Ikiwa unafikiria kuanza kujenga ni vyema ukazingatia mambo haya saba ( 7 ) muhimu ili kufanikisha zoezi la ujenzi kwenda sawia.

1.FEDHA

Kabla ya kuanza ujenzi hakikisha una chanzo kizuri cha mapato ambacho kitakurahisishia shughuli ya ujenzi hivyo kukamilisha nyumba yako kwa wakati.

Pia ni vyema kuwa makini na matumizi ya fedha katika kila hatua ya ujenzi kwani waweza tumia kiasi kikubwa cha fedha bila sababu ya msingi hivyo kujikuta unaishia njiani.

2.MICHORO

Ukiwa tayari una kiwanja chako basi yakupasa kutafuta msanifu majengo (Architect) ambaye atakamilisha suala lote la ujenzi na kukupa ushauri wa kitaalamu kulingana na mahitaji yako unayoyataka.

Ili upate kufahamu michoro inayotakiwa ili upate kibali cha ujenzi ingia hapa

Ili upate kufahamu orodha ya watu wanaohitajika kukamilisha ujenzi wako  ingia hapa.

Wakati wa kubuni ramani yako ni vyema kuwa makini ili upate ramani inayoendana na mtindo wa maisha yako ya kila siku.

3.SHERIA , TARATIBU NA KANUNI

Unapaswa kubaini kuwa si kila kiwanja kinafaa kulingana na mahitaji yako , Huenda wewe unahitaji nyumba ya kawaida tu lakini sheria za mahali kiwanja chako kilipo inataka  pajengwe nyumba za ghorofa moja.

Hivyo waweza kujikuta matatizoni na kushindwa kumaliza ujenzi wako katika muda stahiki. Ni vizuri kuepuka kununua viwanja ambavyo hujui taratibu na malengo ya viwanja husika , kama ni kwa shughuli za makazi au viwanda.

Kumbuka ukizingatia mlolongo huu basi ujenzi kwako utakuwa rahisi mno.

4.MAKADIRIO

Ili uweze kupata picha ya karibu kabisa ni kiasi gani waweza kutumia kufanikisha ujenzi wako unapaswa kupata makadirio katika kila nyanja ya taaluma itakayo husika. Baadhi ya vipengele vya kuzingatia ili kupata makadirio ni –:

                        ( a ) Ujenzi wa nyumba husika

                        ( b)  Gharama ya kutandaza nyaya za umeme ( Wiring) , n.k

Ili kurahisha shughuli hii ya ukadiriaji wa gharama ni vyema ukaonana na mkadiriaji gharama ( Quantity Surveyor ) ili aweze kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa.

5. BIMA YA NYUMBA (HIYARI)

Ili kuepuka kurudi nyuma pindi inapotokea kuzuka kwa moto au majambazi kuvamia eneo lako la ujenzi na kuleta maafa ni vyema ukakata bima ya nyumba yako ili uweze kufidiwa ukikumbwa na majanga kama hayo,

6.KIBALI CHA UJENZI

Baada ya kujiridhisha na gharama za makadirio ya gharama za ujenzi basi waweza songa mbele na kupeleka michoro yako katika mamlaka husika ( manispaa ya mji / jiji ) ili waweze kushughulikia utoaji wa Kibali cha Ujenzi.

Punde upatapo kibali chako utapewa na masharti mbalimbali yatayo tamalaki ujenzi wako.

7.JIANDAE NA UJENZI

Pindi unapokuwa unasubiri kibali kutoka manispaa , waweza kuanza mazungumzo na kampuni za ujenzi ( makandarasi ) mbalimbali ili uweze kuratibu mtirirko wa shughuli ya ujenzi wa nyumba yako.

1 COMMENT

Unknown alisema ...
27 Desemba 2016, 00:16

Mpo vizuri aiissee...!


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506