+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumatano, 8 Oktoba 2014

Vitu kumi na moja (11) vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali cha ujenzi


Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya kuwa na seti ya michoro ya jengo (architectural drawings), hivyo basi kuna vitu vya kuzingatia na ambavyo vinatakiwa kuwepo kwenye michoro hiyo ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza wakati ukitafuta kibali cha kujenga jengo.
Vitu hivyo ni;
1.    Namna jengo litakavyokuwa (plans section, elevation, foundation and roof plan)
Ili kupata kibali cha ujenzi lazima kuwe na michoro itakayoonesha msingi(foundation) utakavyokuwa, mchoro wa kipande/sehemu ya jengo(section plan), paa, na mionekano ya mbele, nyuma, kushoto, na kulia. Michoro yote hii ya namna jengo litakavyokuwa inatakiwa iwe na vipimo vinavyoonekana vizuri.

Mchoro wa jengo (floor plan)

Mchoro wa sehemu ya jengo(section plan)

Mchoro wa paa (roof plan)

Mchoro unaoonesha mionekano ya jengo (elevation)


2.    Namba na eneo la kiwanja kilipo
Hivi huonekana sehemu ya chini au kulia Katika michoro ya namna jengo litakavyokuwa.


3.    Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
Pia sehemu hii huonekana katika michoro yote ya jengo upande wa kulia au chini.

4.    Jina la mchoraji na anwani
Pia hii sehemu huonekana chini au kulia katika michoro ya jengo.


5.    Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
Hii sehemu huonekana kwenye mchoro wa jengo(floor plan) au kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya kiwanja na jengo (site plan).


6.    Ujazo wa kiwanja (plot coverage)
Hii sehemu hueleza ujazo utakao chukuliwa na jengo katika kiwanja, pia huonekana kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya jengo na kiwanja(site plan).


7.    Uwiano (plot ratio)
Hii sehemu hueleza uwiano kati ya jengo na kiwanja, pia huonekana katika mchoro wa site plan.


8.    Matumizi yanayokusudiwa
Hii sehemu hueleza kusudio la matumizi ya jengo, pia huonekana kulia au chini katika michoro yote ya jengo.

9.    Idadi ya maegesho yatakayokuepo
Hii sehemu huonesha idadi ya maegesho ya magari na vitu vingine vinavyozunguka jengo ndani ya kiwanja husika, pia huonekana katika mchoro wa site plan.


10. Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
Hii sehemu hutumika kuonesha umbali uliopo kutoka katika mipaka ya kiwanja mpaka jengo husika, pia huonekana kwenye mchoro wa site plan.


11. Mfumo wa kutoa majitaka hadi kwenye mashimo
Hii sehemu huonesha jinsi ya kutoa majitaka kutoka kwenye jengo mpaka kwenye mashimo ya kuhifadhia,pia sehemu hii huonekana kwenye site plan.


Kutokana na maelezo hapo juu, kwa mtu yeyote anayehitaji kujenga jengo inabidi ahakikishe kila kitu nilichokielezea hapo juu kinaonekana katika seti ya michoro ya jengo (architectural drawings) kabla ya kuendelea na utaratibu mwingine unaofuata.
Kwa maelezo Zaidi wasiliana nami kwenye email; ujenzielekezi04@gmail.com
Usisahau kuweka neno hapo chini

4 COMMENTS

Lugendo ENTERPRISES alisema ...
1 Novemba 2016, 09:56

Ahsante mkuu kwa kutufungua macho


Unknown alisema ...
8 Septemba 2018, 05:04

safi sana nimepata elimu kubwa sana maana nilikuwa natakakufuatilia kibali cha ujenzi wa nyumba yangu,sasa nimejua pakuanzia.


Bila jina alisema ...
5 Februari 2024, 02:22

Ahsante sana kwa msaada wenu kwangu


Bila jina alisema ...
5 Februari 2024, 02:29

Na vipi kuhusu maghorofa


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506