Jumatano, 8 Oktoba 2014
Vitu kumi na moja (11) vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali cha ujenzi
Je Umeipenda Hii Habari?
Kulingana
na sheria ya ujenzi wa majengo mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au
kuanza kujenga jengo bila ya kuwa na seti ya michoro ya jengo (architectural
drawings), hivyo basi kuna vitu vya kuzingatia na ambavyo vinatakiwa kuwepo
kwenye michoro hiyo ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza wakati ukitafuta kibali
cha kujenga jengo.
Vitu
hivyo ni;
1. Namna jengo litakavyokuwa (plans section,
elevation, foundation and roof plan)
Ili kupata kibali cha ujenzi lazima kuwe na
michoro itakayoonesha msingi(foundation) utakavyokuwa, mchoro wa kipande/sehemu
ya jengo(section plan), paa, na mionekano ya mbele, nyuma, kushoto, na kulia.
Michoro yote hii ya namna jengo litakavyokuwa inatakiwa iwe na vipimo
vinavyoonekana vizuri.
Mchoro wa
jengo (floor plan)
Mchoro wa
sehemu ya jengo(section plan)
Mchoro wa
paa (roof plan)
Mchoro
unaoonesha mionekano ya jengo (elevation)
2. Namba na eneo la kiwanja kilipo
Hivi huonekana sehemu ya chini au kulia Katika
michoro ya namna jengo litakavyokuwa.
3. Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
Pia sehemu hii huonekana katika michoro yote ya
jengo upande wa kulia au chini.
4. Jina la mchoraji na anwani
Pia hii sehemu huonekana chini au kulia katika
michoro ya jengo.
5. Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
Hii sehemu huonekana kwenye mchoro wa
jengo(floor plan) au kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya kiwanja na
jengo (site plan).
6. Ujazo wa kiwanja (plot coverage)
Hii sehemu hueleza ujazo utakao chukuliwa na
jengo katika kiwanja, pia huonekana kwenye mchoro unaoonesha mpangilio kati ya
jengo na kiwanja(site plan).
7. Uwiano (plot ratio)
Hii sehemu hueleza uwiano kati ya jengo na
kiwanja, pia huonekana katika mchoro wa site plan.
8. Matumizi yanayokusudiwa
Hii sehemu hueleza kusudio la matumizi ya jengo,
pia huonekana kulia au chini katika michoro yote ya jengo.
9. Idadi ya maegesho yatakayokuepo
Hii sehemu huonesha idadi ya maegesho ya magari
na vitu vingine vinavyozunguka jengo ndani ya kiwanja husika, pia huonekana
katika mchoro wa site plan.
10. Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja
(setbacks)
Hii sehemu hutumika kuonesha umbali uliopo
kutoka katika mipaka ya kiwanja mpaka jengo husika, pia huonekana kwenye mchoro
wa site plan.
11. Mfumo wa kutoa majitaka hadi kwenye mashimo
Hii sehemu huonesha jinsi ya kutoa majitaka
kutoka kwenye jengo mpaka kwenye mashimo ya kuhifadhia,pia sehemu hii huonekana
kwenye site plan.
Kutokana
na maelezo hapo juu, kwa mtu yeyote anayehitaji kujenga jengo inabidi
ahakikishe kila kitu nilichokielezea hapo juu kinaonekana katika seti ya
michoro ya jengo (architectural drawings) kabla ya kuendelea na utaratibu
mwingine unaofuata.
Usisahau
kuweka neno hapo chini
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
4 COMMENTS
1 Novemba 2016, 09:56
Ahsante mkuu kwa kutufungua macho
8 Septemba 2018, 05:04
safi sana nimepata elimu kubwa sana maana nilikuwa natakakufuatilia kibali cha ujenzi wa nyumba yangu,sasa nimejua pakuanzia.
5 Februari 2024, 02:22
Ahsante sana kwa msaada wenu kwangu
5 Februari 2024, 02:29
Na vipi kuhusu maghorofa
Chapisha Maoni