Jumatano, 29 Julai 2015
Kuna sababu mbalimbali zilizopelekea binadamu kubadilisha mifumo ya kuishi (life style) na hii imesababisha mabadiliko makubwa sana katika upande wa ujenzi tokea kuishi kwenye vichaka na miamba/mapango mpaka sasa kwenye majengo. Hivyo basi hatuna budi kukupa historia za tamaduni zetu na maeneo waliyoishi miaka hiyo na kama ukivutiwa zaidi unaweza tembelea (utalii wa ndani).
Jumanne, 28 Julai 2015
-
Anza na neno ujenzielekezi
-
Jina lako kamili mfano juhudi maendeleo
-
Aina ya ufundi mfano fundi rangi, kwa wale madalali andika dalali
-
Mkoa ulipo mfano Pwani
Jumamosi, 25 Julai 2015
Karibu sana mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi. Leo tunaendelea na mfululizo wa makala zetu za ujenzi kama ilivyoada.Leo tunaangazia kuhusu Sauna au Bafu mvuke. Huenda ulishawahi kusikia kuhusu hili neno au kupata kutumia kabisa chumba hiki.Sauna huweza kujengwa nje ya jengo kuu au likawa ndani ya jengo kuu.
Sauna au ( Bafu la mvuke kwa Kiswahili ) ni Chumba kidogo au jengo lililosanifiwa / buniwa kama sehemu ya kupata joto la mvuke. Mvuke ambao huweza kuwa mkavu au wenye maji maji.
Ambapo mvuke na joto la hali ya juu huwafanya watu kutoka jasho.
Sauna huweza kugawanyika katika Makundi mawili.
1.BAFU MVUKE LA KAWAIDA / ASILI :
Hii ni sauna ambayo huipa hewa joto na kisha hewa kusambaa katika chumba na kuipasha ngozi.Sauna hii hupitisha joto kwa njia ya uoevu (convection).
2.BAFU MVUKE LA MIALI:
Hii ni sauna ambayo hupasha vitu joto moja kwa moja.
Bafu mvuke la miali hutumia nyenzo mbali mbali kwa ajili ya kupasha joto kama vile mkaa, nyuzi nyuzi hai za kaboni na nyenzo nyingine nyingi.
UTENDAJI KAZI WA SAUNA:
Jotoridi ambalo hukaribia 100oc (212o F) Litakuwa moja kwa moja halivumiliki kabisa.
Sauna huwekewa madirisha madogo kiasi yenye matundu ambayo huruhusu hewa kuingia ili watumiaji wapate kupumua vyema.
FAIDA ZA KIAFYA ZA SAUNA:
1.Matumizi ya sauna huweza kutuliza dalili za mwili kujisikia baridi.
2.Pia kupunguza hamu ya kula na hivyo kupunguza uzito wa mwili.
3.Hupunguza uchovu wa mwili.
4.Pia hupendekezwa kutumiwa kwaajili ya kurudisha nguvu baada ya mzazi kujifungua.
5.Hupunguza / huondoa msongo wa mawazo.
6.Husafisha ngozi
7.Huleta usingizi mzito
8.Hupoza misuli na kupunguza maumivu kwenye maungio
MADHARA YA MATUMIZI YA SAUNA:
1.Watu wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo au walevi na wateja wa madawa ya kulevya huwa hatarini wakitumia sauna.
2.Matumizi ya Sauna yamethibitika kupelekea upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.Kumekuwa na ushahidi kuwa joto limekuwa na athari katika uzalishaji wa mbegu za kiume.
USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
-
Jokofu (refrigerator)
-
makabati (shelves or cupboard)
-
Meza (table)
-
Sink
-
jiko la kupikia (stove or range)
-
kabati la juu (shelves)
Jumatano, 22 Julai 2015
sasa hapa tuangalie baadhi ya picha zinazoonesha urembo katika majengo uliotumia matairi mabovu ya magari kama malighafi.
UREMBO UNAOVUTIA ULIOTENGENEZWA KWA TAIRI
Jumamosi, 18 Julai 2015
Wakati mwingine watu hawapendi kukaa nyumbani kwa sababu kuna vitu havipo nyumbani mfano mtu ni mwanamichezo na kwake hata sehemu ya kuruka kamba haipo Je atapata vipi hamu ya kukaa nyumbani? hivyo basi ni vizuri ukiwa unafikiria kujenga nyumba ya kuishi kuangalia na mahitaji ya nafasi yako katika jamii mbali na yale tuliyozoea kama vile vyumba vya kula.
Hapa tumekuandalia picha zinazoonesha baadhi ya maeneo ya nyumba wanayokaa wasanii wakubwa duniani yaani Jay Z na Beyonce yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 43 kwa lengo la kukuonesha ni vitu/sehemu gani ambazo wao walizipa kipaumbele kuzipendezesha ili kufanya mazingira yawe rafiki na sifa zao.
-
sehemu ya mbele (front)
-
sehemu ya nyuma
-
ina vyumba vya kulala 12
-
maktaba
-
chumba cha faragha (closet) cha aina yake
-
chumba cha kucheza mchezo wa kitufe (bowling)
-
sehemu ya kucheza tennis
-
chumba cha habari (media room)
-
chumba cha tv (tv room)
-
chumba cha michezo
-
chumba cha mazoezi (gym)
-
bafu la mvuke (sauna)
-
sehemu ya kuogelea (pool)
Ijumaa, 17 Julai 2015
Kwanza kabisa utengenezaji mzuri wa mpangilio wa mazingira yanayokuzunguka husaidia vitu vingi kama kuua wadudu wanaokaa sehemu zenye uchafu, kurahisisha upitaji, kuboresha afya, na pia ni urembo.
Mbali na sifa za kutengeneza mazingira hapo juu pia kama utaweza kutengeneza vizuri inaweza kuwa fursa ya ajira maana si kila mtu anaeweza wengine huomba kusaidiwa. Pia zipo hadi kampuni zinazotoa huduma hii.
Alhamisi, 16 Julai 2015
Kabla ya yote bonyeza maandishi ya bluu hapo chini ili kusoma habari zilizokwisha wekwa ambazo zinaweza kukusaidia
vitu vya kuchunguza kabla hujanunua kiwanja
Kabla hujafikiria kujenga zingatia haya
Vitu 11 vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali
Jumatano, 15 Julai 2015
Habari za wakati mpedwa msomaji! yaweza kuwa mpaka sasa unajiuliza ni vigae gani unataka kutumia kwenye sehemu/vyumba vya jengo lako mfano sebuleni, jikoni, vyumba vya kulala, stoo, chooni, bafuni, nk. Basi majibu yake yapo hapo chini.
Aina za vigae
Kuna aina mbili za vigae
1. kutokana na malighafi/material iliyotengeneza mfano ceramic, marble, slate, porcelain, granite,carpet , nk.
picha ya vigae vya ceramic
2. kutokana na umbile (texture) – hapa kuna aina mbili vinavyokwaruza(grazed) na visivyokwaruza (ungrazed)
picha ya vigae vinavyokwaruza (grazed)
Sababu za kufuata ukiwa unachagua vigae vya kusakafia
1. Matumizi ya eneo husika – Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala
2. Upatikanaji – kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine iliyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.
3. Uwezo wake na muda wa kuaribika – vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.
4. Gharama (mfuko wako) – ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.
Zingatia: sababu hizi ni za msingi(basic) kwa yule anayehitaji vigae. kwa msaada zaidi onana na wataalamu husika kama wasanifu majengo(architect) au wakadiliaji ujenzi (quantity surveyor)
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965