Alhamisi, 21 Mei 2015
zifahamu kazi na wajibu wa msanifu majengo katika ujenzi
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi, ni kawaida yetu kukusalimu na kukuombea mema kila wakati. Mungu akubariki sana kwa kuweza kuingia kwenye blog hii kwa maana upo sehemu sahihi inayokupa muelekeo wa kiujenzi.
Ni matumaini yetu kuwa kila atakaesoma hii habari, moja itamsaidia kujua ni mtaalamu gani wa kwanza kuonana nae pale linapokuja wazo la kujenga, na mbili itasaidia kuwafafanulia wale wote wanaotaka kusomea fani hii.
Usanifu majengo(architecture) ni sayansi na sanaa ya kubuni na kufanya mpangilia wa majengo. Majengo hayo ni kama majengo ya kuishi(residential), ya kibiashara (business), historia (museum), na viwanda (industrial). watu/mtu mwenye utaalamu huu anaitwa msanifu majengo (architect).
kazi/majukumu ya msanifu majengo(architect)
- Kubuni na kufanya mpangilio wa jengo – kazi hii huifanya kwa kusikiliza kwanza mahitaji ya mteja(client).
- kutengeneza michoro ya jengo – michoro hii ni kama tulivyoielezea kwenye habari hii http://ujenzielekezi.blogspot.com/2014/10/vitu-kumi-na-moja-11-vya-kuzingatia_76.html
- na kusimamia jengo (kuhakikisha kile kilichochorwa ndicho kitakachojengwa
kujua watu wengine wenye ujuzi wanaohusika kwenye ujenzi ingia hapa
http://ujenzielekezi.blogspot.com/2014/11/hii-ndiyo-orodha-ya-watu-wanaohusika.html
kwa wale wanaotaka kusomea ujuzi/fani hii kwa hapa tanzania,
- Ngazi ya astashahada/grade inatolewa na baadhi ya vyuo vya VETA.
- Ngazi ya stashahada/diploma inatolewa Mbeya University of Science and Technology(MUST).
- Ngazi ya shahada/degree inatolewa Mbeya University of Science and Technology(MUST), Ardhi University(ARU), na University of Dar-es-salaam(UDSM).
kwa maoni/ushauri/msaada wasiliana nasi kupitia email yetu ujenzielekezi04@gmail.com
1 COMMENT
19 Januari 2021, 12:10
Je? Iliuwe na sifa ya kusoma stashahada ya ubunifu majengo natakiwa uwe na sifa zipi?
Chapisha Maoni