+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumanne, 26 Mei 2015

zifahamu kazi na wajibu wa mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor) katika ujenzi

3

Habari za wakati huu mpendwa msomaji, ahsante kwa kuendelea kuwa sehemu sahihi inayokupatia taarifa mbali mbali zinazohusu ujenzi. Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine zaidi zinazokuja.

Mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor/ building economy) ni mtaalamu anaefuatia baada ya mtaalamu anaehusika na ubunifu na uchoraji (msanifu majengo) kumalisha kazi ya kutengeneza michoro.

http://ujenzielekezi.blogspot.com/2015/05/zifahamu-kazi-na-wajibu-wa-msanifu.html

Kazi/wajibu wa mkadiliaji ujenzi (quantity surveyor)

Kwa kufuata michoro iliyochorwa kazi na wajibu wa mkadiliaji ujenzi ni;

  • Kufanya makadilio ya gharama ya jengo kwanzia mwanzo hadi mwisho, kwa kuzingatia malighafi(material) yaliyopendekezwa na msanifu majengo(architect)

property builder project

  • Kuandaa hati ya vipimo na gharama (bills of quantity)

image

  • kuandaa na kupitia mikataba ya uzabuni (tender documents)

4

  • kuandaa ripoti za fedha (financial report)

2

  • kutoa ushauri wa mambo ya gharama za ujenzi, mfano vifaa, malighafi, nk.

kwa wale wanaotaka kusomea utaalamu huu ngazi ya shahada (degree/bachelor) kwa Tanzania inatolewa ardhi university(ARU).

Na kwa wale wenye michoro wanataka kujua gharama za ujenzi, au wale wanaotaka kufanyiwa Tathmini ya gharama za majengo yao BASI hawa ndiyo dawa ya matatizo hayo.

Kufahamu wataalamu wengine wanaohusika bonyeza maandishi hayo ya bluu hapo chini

http://ujenzielekezi.blogspot.com/2014/11/hii-ndiyo-orodha-ya-watu-wanaohusika.html

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia

email: ujenzielekezi04@gmail.com

Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

 

 

Jumatatu, 25 Mei 2015

hivi ndiyo vitu vinavyofanya bei ya viwanja iwe juu au chini

IMG_7433

Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa makala zetu za ujenzi tunatumaini tunakupatia taarifa nzuri zenye kukuelimisha kuhusu ujenzi, endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi juu ya mambo ya ujenzi.

Mpendwa msomaji hivi umeshawahi kujiuliza kwanini bei ya viwanja inatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine? au unakiwanja/viwanja unataka kuuza ushawahi kufikiria ni vitu gani vya kwanza kuangalia ili kutambua bei ya kiwanja/viwanja vyako? Jibu sahihi ni hili hapo chini.

Vitu vinavyoleta utofauti wa bei za viwanja kutoka sehemu moja hadi nyingine 

  1. Miundombinu – hapa tunamaanisha barabara, mifumo ya umeme, maji safi na majitaka. Hivyo basi viwanja ambavyo miundombinu hii hupatikana kiurahisi huwa vina bei ya juu ukilinganisha na viwanja ambavyo miundombinu hii haipatikani kirahisi.IMG_0025
  2. Asili(nature) ya eneo – Hapa tunamaanisha miinuko na udongo, yaani viwanja ambavyo huwa katika sehemu iliyoinuka (slope) huwa bei chini. Vile vile na viwanja ambavyo vipo kwenye udongo wa kichanga huwa bei chini.IMG_7447
  3. Huduma za kijamii – hii ndiyo iliyozoeleka na wengi kwamba viwanja ambavyo vipo karibu na huduma za kijamii mfano shule, soko, duka, barabara kuu, nk. huwa vinagharama kubwa.IMG_0022
  4. Majirani – Mara nyingi sifa hii inategemea eneo na eneo, yaani viwanja ambavyo vipo maeneo ambayo hayajatulia(uswailini) huwa bei chini mfano kwa wale wanaokaa dar-es-salaam kiwanja ambacho kipo maeneo ya masaki au mbezi beach huwa bei juu ukilinganisha na kile ambacho kipo buguruni au tandareIMG_0027
  5. Vipimo – Viwanja ambavyo vipo maeneo ambayo yamepimwa huwa bei ya juu ukilinganisha na vile ambavyo vipo maeneo ambayo hayajapimwa
  6. muonekano wa mnunuaji – japo hii sio sana lakini huzingatiwa na muuzaji, mfano bei atakayotajiwa mtu wa kawaida inaweza kuwa tofauti na atakayotajiwa mtu kama mkurugenzi, meneja wa kampuni flani.

NB. Ukiona kiwanja/viwanja vinauzwa bei ya juu na hivyo vitu hapo juu vinavyoonesha sifa ya kiwanja kuwa bei juu havijazingatiwa basi jua kwamba unapigwa

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia email hii ujenzielekezi04@gmail.com

Jumamosi, 23 Mei 2015

KABLA HUJAFIKIRIA KUJENGA ZINGATIA HAYA

Kwa kawaida ukifikiria kujenga huwa huwazi juu ya hali ya hewa na wala hufikirii kuhusu nyenzo / materials za ujenzi kama zitakuwa kikwazo katika ujenzi wako.

Katika tovuti hii tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali za ujenzi ili kukufumbua macho zaidi na kurahisisha shughuli ya ujenzi kwako.

Ikiwa unafikiria kuanza kujenga ni vyema ukazingatia mambo haya saba ( 7 ) muhimu ili kufanikisha zoezi la ujenzi kwenda sawia.

1.FEDHA

Kabla ya kuanza ujenzi hakikisha una chanzo kizuri cha mapato ambacho kitakurahisishia shughuli ya ujenzi hivyo kukamilisha nyumba yako kwa wakati.

Pia ni vyema kuwa makini na matumizi ya fedha katika kila hatua ya ujenzi kwani waweza tumia kiasi kikubwa cha fedha bila sababu ya msingi hivyo kujikuta unaishia njiani.

2.MICHORO

Ukiwa tayari una kiwanja chako basi yakupasa kutafuta msanifu majengo (Architect) ambaye atakamilisha suala lote la ujenzi na kukupa ushauri wa kitaalamu kulingana na mahitaji yako unayoyataka.

Ili upate kufahamu michoro inayotakiwa ili upate kibali cha ujenzi ingia hapa

Ili upate kufahamu orodha ya watu wanaohitajika kukamilisha ujenzi wako  ingia hapa.

Wakati wa kubuni ramani yako ni vyema kuwa makini ili upate ramani inayoendana na mtindo wa maisha yako ya kila siku.

3.SHERIA , TARATIBU NA KANUNI

Unapaswa kubaini kuwa si kila kiwanja kinafaa kulingana na mahitaji yako , Huenda wewe unahitaji nyumba ya kawaida tu lakini sheria za mahali kiwanja chako kilipo inataka  pajengwe nyumba za ghorofa moja.

Hivyo waweza kujikuta matatizoni na kushindwa kumaliza ujenzi wako katika muda stahiki. Ni vizuri kuepuka kununua viwanja ambavyo hujui taratibu na malengo ya viwanja husika , kama ni kwa shughuli za makazi au viwanda.

Kumbuka ukizingatia mlolongo huu basi ujenzi kwako utakuwa rahisi mno.

4.MAKADIRIO

Ili uweze kupata picha ya karibu kabisa ni kiasi gani waweza kutumia kufanikisha ujenzi wako unapaswa kupata makadirio katika kila nyanja ya taaluma itakayo husika. Baadhi ya vipengele vya kuzingatia ili kupata makadirio ni –:

                        ( a ) Ujenzi wa nyumba husika

                        ( b)  Gharama ya kutandaza nyaya za umeme ( Wiring) , n.k

Ili kurahisha shughuli hii ya ukadiriaji wa gharama ni vyema ukaonana na mkadiriaji gharama ( Quantity Surveyor ) ili aweze kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa.

5. BIMA YA NYUMBA (HIYARI)

Ili kuepuka kurudi nyuma pindi inapotokea kuzuka kwa moto au majambazi kuvamia eneo lako la ujenzi na kuleta maafa ni vyema ukakata bima ya nyumba yako ili uweze kufidiwa ukikumbwa na majanga kama hayo,

6.KIBALI CHA UJENZI

Baada ya kujiridhisha na gharama za makadirio ya gharama za ujenzi basi waweza songa mbele na kupeleka michoro yako katika mamlaka husika ( manispaa ya mji / jiji ) ili waweze kushughulikia utoaji wa Kibali cha Ujenzi.

Punde upatapo kibali chako utapewa na masharti mbalimbali yatayo tamalaki ujenzi wako.

7.JIANDAE NA UJENZI

Pindi unapokuwa unasubiri kibali kutoka manispaa , waweza kuanza mazungumzo na kampuni za ujenzi ( makandarasi ) mbalimbali ili uweze kuratibu mtirirko wa shughuli ya ujenzi wa nyumba yako.

Alhamisi, 21 Mei 2015

zifahamu kazi na wajibu wa msanifu majengo katika ujenzi

3

Habari za wakati huu mpenzi msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi, ni kawaida yetu kukusalimu na kukuombea mema kila wakati. Mungu akubariki sana kwa kuweza kuingia kwenye blog hii kwa maana upo sehemu sahihi inayokupa muelekeo wa kiujenzi.

Ni matumaini yetu kuwa kila atakaesoma hii habari, moja itamsaidia kujua ni mtaalamu gani wa kwanza kuonana nae pale linapokuja wazo la kujenga, na mbili itasaidia kuwafafanulia wale wote wanaotaka kusomea fani hii.

Usanifu majengo(architecture) ni sayansi na sanaa ya kubuni na kufanya mpangilia wa majengo. Majengo hayo ni kama majengo ya kuishi(residential), ya kibiashara (business), historia (museum), na viwanda (industrial). watu/mtu mwenye utaalamu huu anaitwa msanifu majengo (architect).

kazi/majukumu ya msanifu majengo(architect)  

  • Kubuni na kufanya mpangilio wa jengo – kazi hii huifanya kwa kusikiliza kwanza mahitaji ya mteja(client).

1

2

  • na kusimamia jengo (kuhakikisha kile kilichochorwa ndicho kitakachojengwa

4

kujua watu wengine wenye ujuzi wanaohusika kwenye ujenzi ingia hapa

http://ujenzielekezi.blogspot.com/2014/11/hii-ndiyo-orodha-ya-watu-wanaohusika.html

kwa wale wanaotaka kusomea ujuzi/fani hii kwa hapa tanzania,

  1. Ngazi ya astashahada/grade inatolewa na baadhi ya vyuo vya VETA.
  2. Ngazi ya stashahada/diploma inatolewa Mbeya University of Science and Technology(MUST).
  3. Ngazi ya shahada/degree inatolewa Mbeya University of Science and Technology(MUST), Ardhi University(ARU), na University of Dar-es-salaam(UDSM).

kwa maoni/ushauri/msaada wasiliana nasi kupitia email yetu ujenzielekezi04@gmail.com

Jumatano, 20 Mei 2015

JINSI YA KUANDAA MAZINGIRA YA KUCHOREA kwenye program ya autocad

autocad-logo
Katika sehemu ya kwanza tumeona vitu vinavyoonekana ukifungua program ya AutoCAD kwa mara ya kwanza, katika sehemu hii ya pili tunaenda kuangalia maandalizi unayotakiwa kufanya kabla hujaanza kuchora.
Unapofungua AutoCAD kwa mara ya kwanza kuna baadhi ya toolbar huonekana kama tulivyozielezea kwenye sehemu ya kwanza, lakini vilevile kuna ambazo zimejificha (hide) ambazo hazionekani mpaka uzitafute zilipo.
Jinsi ya kuzirudisha/kuzifungua toolbar ambazo zimejificha.
kuna njia mbili:
1. unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye sehemu iliyowazi(blank area) yaani ambayo haina toolbar yeyote, unabonyeza kitufe cha kulia(right click) cha kipanya(mouse), unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye sehemu iliyoandikwa ACAD, hapo usibonyeze itakuletea yenyewe orodha ya toolbar zote zilizokuwa zimefichwa na ambazo zinaonekana ulipofungua program
NB. Zilizowekewa alama ya pata ndizo zinazoonekana kwenye program na ambazo hazijawekewa ndiyo ambazo zimejificha kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini
clip_image002
2. Hii ndiyo nyepesi Zaidi, unapeleka mshale(kwa kutumia kipanya) kwenye ikoni yeyote iliyokwenye toolbar yeyote mfano toolbar ya kuchorea (draw toolbar) katika ikoni ya mstari (line icon), kisha unabonyeza kitufe cha kulia (right click) cha kipanya, hapo tayari itakuletea orodha ya toolbar zote ambazo zimefichwa na ambazo hazijafichwa kama invyoonekana kwenye picha hapo chini.
clip_image004

Jumanne, 19 Mei 2015

LIFAHAMU JENGO LA KIHISTORIA LA TAJ MAHAL


--------------------------------------------------------------------------------



     Miongoni mwa vivutio vikubwa ulimwenguni ni jengo la kitamaduni la Taj Mahal.
Ambalo hupata kutembelewa na watalii takribani milioni 3 kila mwaka.
Lipo Agra nchini India lina urefu upatao m 73 (ft 240).
    Kitu kikubwa kiwavutiacho watu ni historia ya jengo hili na kisa cha ujenzi wake ukiachilia mbali ubora wa nyenzo / materials zilizo tumika kwenye ujenzi huu kwani ni jengo la muda mrefu lakini bado lipo kwenye wakatiwa  kisasa na linavutia machoni mwa watu.



Aina ya Mtindo wa kisanifu uliotumika ni Mughal Architecture
Inaaminika kuwa Taj Mahal ( hutafsiriwa kama Taji la Himaya ) ni ufupisho wa jina la Mumtaz Mahal (Aliyefahamika zaidi kama Arjumand Bano Begum).
     Ujenzi huu ambao ulitumia zaidi nyenzo za marble nyeupe , uligharamiwa na mfalme Shah Jahan (1628-1658) ambaye alijenga jengo hili ili kuenzi fikra za mke wake kipenzi miongoni mwa wake zake watatu , Mumtaz Mahal (aliyefariki mwaka 1630 AD alipokuwa akijifungua mtoto wao wa 14 , Gauhara Begum ) ambaye aliwahi kuwaza kujenga kaburi (tomb) kama dunia ambalo hakuwahi kuliona kabla.



 Ujenzi wa Taj Mahal ulianza mwaka 1632 AD na kumalizika mwaka 1653 AD.
Ujenzi wa jengo pekee ulikamilika mwaka 1648 ila ujenzi wa Mazingira ya nje ulikamilika 1653.
      Kwa miaka 21 watu takribani 20,000 walipata kuajiriwa kukamilisha ujenzi huu.
Ili kuweza kutoa huduma za malazi kwa waajiriwa hawa , Mji mdogo wa Taj Ganj ulianzishwa kwa ajili hiyo.
Na mbunifu wa Taj Mahal ni Ustad Ahmad Lahauri ambaye asili yake ni Pakistan.
Kuba / Dome la katikati lina urefu wa futi 240 ,sawa na mita 73.

Jumatano, 13 Mei 2015

JINSI YA KUPENDEZESHA USO WA MBELE WA NYUMBA ( FRONT FACADE)

Pasi na shaka ndaniye, Kitu cha kwanza ambacho mgeni wako anapaswa kukitanabahi pindi ajapo kwako ni kuona uso wa nyumba ambao utamkaribisha kwa bashasha tele.
Hivyo kuna kila sababu ya kutumia nguvu kubwa kutengeneza uso wa mbele wa nyumba.
Kuna nyumba nyingine zimekosa muonekano mzuri wa mbele hivyo husababisha kushindwa kutofautisha uso wa mbele na uso wa nyuma wa nyumba au na upande wa kulia na kushoto.
Hivyo Msanifu wa majengo hana budi kutumia maarifa kuandaa ramani ambayo itakidhi mahitaji ya Nyumba husika.


BAADHI YA SEHEMU AMBAZO UNAWEZA KUPENDEZESHA KWENYE NYUMBA.
1. Nguzo
Hii ni moja ya sehemu ya jengo ambayo ni nyoofu. Inaweza ikawa ya umbo la duara au,mstatili au mraba kulingana na mahitaji yako.
Aina tofauti za usanifu zaweza tumiwa ili kukidhi haja ya mahitaji husika.
Mitindo itumiwayo sana kwenye nguzo ni pamoja na Doric , Ionic na Corinthian ambapo usanifu mwingine huweza kuchukua nafasi hapa.





2. Urembo Kwenye Archs
Unaweza ukaambatanisha na Keystone au Ukaacha hivi hivi na bado Arch ikawa nzuri tu.
Tumia nyenzo/ material ambazo ni rafiki wa mvuto kwa macho.


3. Madirisha
Kwakutegemea na vigezo vya sehemu au sababu za kisanifu, Msanifu ataweza kupendekeza aina ya dirisha kwa kutegemea anataraji kuweka athari kwenye nini i.e unyoofu (verticality ) au mlalo ( horizontality).

4. Milango Ya Nje
Aina mbali mbali za milango hutumiwa kwa kuzingatia aina ya mtiririko (pattern) sanifu wa msanifu ili kutokupoteza mtiririko mzima wa umoja wa mtindo wa mpangilio  wa jengo ulivyochaguliwa.

5.Kuta
6. Nakshi nyingine za Kisanifu
Nakshi nyingine ni kama vile Quoin ambayo huweza kutumika kwenye kona za pembe ya nyumba.














Jumamosi, 9 Mei 2015

ZIFAHAMU AINA MBALIMBALI ZA ROOFING MATERIALS


Kabla hujaanza ujenzi ni vyema ukabaini ni aina gani ya bati utaezeka kwenye nyumba yako.
Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kuamua aina ya ezekeo ulitalo kwenye nyumba yako:

1. Gharama ya aina ya Ezeko/Roof husika
2. Upatikanaji wake
3. Uimara wake / durability
4. Hali ya hewa i.e Uwezo wake kuhimili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ya mahali husika.
5. Mvuto / Aesthetics.
6. Salama kwa afya.
7. Rafiki wa mazingira 

AINA ZA ROOFING MATERIALS AMBAZO ZINATUMIKA SANA SIKU HIZI

1. Roof Tiles (Ezeko la Vigae)

Mara nyingi hivi vigae hutengenezwa kwa udongo / clay tiles au zege /concrete tiles.
Ikumbukwe vigae vya udongo vilianza kutumika zamani sana kabla ya concrete tiles na hudumu kwa takribani miaka 50 hadi 100. Ila mbao zilizoshikilia vigae / battens & underlayments hudumu kwa takribani miaka 5-15 pekee.

vigae vya udongo/clay tiles

vigae vya zege jepesi/lightweight-concrete tiles


2. Metal Sheets
Hizi ni paa ambazo hutengenezwa kwa metali katika viwanda kwa kupitia michakato mbalimbali ambayo mwishowe huzalisha bati nyembamba na nyoofu kabisa ambazo huwekwa katika maumbo na aina tofauti tofauti ili kukidhi uhitaji wa wanunuzi.

Faida ya kutumia metal sheets ni pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili hali mbaya ya hewa na kutoa ulinzi mathubuti kwa jengo lako. Metal Sheets
huweza kudumu hadi kwa miaka 50 ila itabidi uangalie fasteners kwa kila baada ya miaka 2 ili uweze kubaini kama zinahitajika kubadilishwa au la. Hii ni muhimu katika kuboresha umadhubuti wa utendaji kazi wa paa lako.

MATERIALS:

  • Stainless steel
  • Aluminium
kupata kufahahamu zaidi Ubora na Gage wa stainless steel na aluminium soma hapa



metal sheets


IT 5 SHEETS




Jumapili, 3 Mei 2015

je unataka kujifunza autocad? ingia hapa.

UTANGULIZI

AutoCAD ni moja ya program au software inayotumiwa na wahandisi, wasanifu majengo, wachoraji, wapima ramani, nk. Kwa ajili ya kuchorea. Kutokana na kukua kwa utandawazi program hii imeweza kusaidia watumiaji kuondoka katika mifumo ya kuchora kwa mkono. Ukiachana na kuwepo kwa program hii kuna program nyingine nyingi ambazo hutumika kuchorea nazo ni kama Arch Cad, vector, home sweet designer, nk. Lakini zimeonekana kuwa ngumu kutumia na kuwa na vitu visivyokidhi mahitaji ya wengine.

MWANZO (SEHEMU YA KWANZA)

Unapokuwa umekwisha iweka(install) program hii kwenye computer yako ukiifungua itaonekana kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

5

 

No.

JINA

KAZI

1.

Title bar

Kuonesha jina la mchoro uliofunguliwa kutokana na jinsi ulivyotunzwa(save) mf. Document 1. Na sehemu inayofunga(close), kupunguza (restore), na kufunika mchoro(minimize/maximize)

2.

Menu bar

Kuonesha vitu vyote vinavyomsaidia mtumiaji kutumia katika program hii mf. File,view,edit, nk.

3.

Standard toolbar

Kuonesha vitufe ambavyo hutumiwa mara nyingi na mtumiaji mf. New, open, save, nk.

4.

Styles

Kuonesha aina ya maneno(text), vipimo(dimension), na table. Mara nyingi huandika standard.

5.

Workspaces

Kuonesha aina ya sehemu ya kuchorea inaweza kuwa vipimo viwili(2 dimension) au vipimo vitatu(3 dimension) mf. 3d modelling, au autocad classic

6.

Layers

Kuonesha aina ipi ya maandishi uliyoitengeneza unayoitumia.

7.

Properties

Kuonesha aina ipi ya unene/rangi uliyoitengeneza unayoitumia.

8.

Draw toolbar

Huonesha vitufe vinavyotumika kutengenezea mchoro mf. Line, rectangular, arch, nk.

9.

Modify toolbar

Huonesha vitufe vinavyotumika kufanyia marekebisho au niongeza ya vitu vilivyochorwa mf. Erase, trim, offset, nk.

10.

Dimension toolbar

Huonesha vitufe vinavyomika kupima vitu vilivyochorwa mf. Linear dimension, radius, diameter, nk.

11.

Layout

Huonesha mazingira ya kuchorea(model)/ kuchapia(print) mchoro mf. Model, layout 1, nk.

12.

Info toolbar

Huonesha maelekezo unayofuata baada ya kubonyeza kitufe chochote.

13.

Status toolbar

Huonesha maelezo ya kimahesabu yaliyopo sehemu ya kuchorea pamoja na vitufe vinavyotumika kuongeza ufanisi katika kuchora mf. Ortho, osnap, line weight type, nk.

14

Working area

Hii ndiyo sehemu ya kuchorea

NB. Pia unaweza kufungua kwa mara ya kwanza program ya autocad lakini ukakuta vitu hivi vimepungua. Jinsi ya kuvirudisha na kuona vingine fuatilia sehemu ya pili.

Ijumaa, 1 Mei 2015

JINSI YA KUANDAA DOORS & WINDOWS SCHEDULE KWENYE ARCHICAD


   Utangulizi & Historia ya Interactive Schedule

ArchiCAD’s Interactive Schedule Inakuruhusu uweze kuandaa DOORS & WINDOWS SCHEDULE Haraka na Kwa Urahisi Sana.Interactive Schedule Inaonyesha Idadi ya elements zilizotumika, Pia inakuruhusu uweze kufanya marekebisho ya element husika.Hii inakusaidia kuweza kubaini kama kulikuwa na  makosa kwenye kuweka data za element husika.
Kwa mfano Interactive Schedule inaweza kukuonyesha katika madirisha yote yaliyoweka kuwa yana urefu sawa na upana sawa. Hivyo waweza kulichagua dirisha husika na kulifanyia marekebisho na itakuwa "updated" mara moja.
  

kuandaa  door au window schedule Utatumia Element List . Nenda kwenye  Navigator > Project Map > shuska chini hadi kwenye Schedules > Element > chagua Door List auWindow List

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506