Photo by: Flickr

Bidhaa

za ujenzi

Soma Zaidi
Photo by: Flickr

Huduma

Ya mafundi ujenzi

Soma Zaidi
Photo by: Flickr

Ushauri

Wa Ujenzi

Soma Zaidi

We are Unique Experts

Huduma

kwa mahitaji ya mafundi wa nyumba(kuona kazi zao na mawasiliano) bonyeza hapa..

Bidhaa

bonyeza hapa.. kuona bidhaa mbalimbali zinazotumika katika ujenzi wa nyumba

Ushauri

kwa ushauri na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi wa nyumba bonyeza hapa ..

Awesome

bonyeza hapa.. kuona picha na video za ubunifu wa nyumba na majengo mengine.

Taarifa

bonyeza hapa.. kujua viwanja na nyumba zinazouzwa au kupangishwa

Historia

karibu katika kipengele hiki kujua historia mbalimbali zinazohusu ujenzi.

+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Jumatano, 9 Mei 2018

Picha za design ya nyumba na muonekano wa nje (landscape) yenye kiwanja chenye ukubwa wa mita 15 kwa 35



Habari za wakati ndugu msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi wa majengo! Katika makala hii tunakuonesha picha za moja ya design mazingira ya nje na jengo kulingana na ukubwa wa kiwanja ulichonacho.


  • nyumba inaukubwa wa mita 11.1 kwa 12.6 na
  • kiwanja kinaukubwa wa mita 15 kwa 35
 muonekano wa mbele nje ya fensi

muonekano wa mbele ya nyumba ambapo ni eneo la maegesho ya magari

eneo la nyuma (kuingilia mlango wa nyuma)

eneo la nyuma ambapo ni pakufulia na kuanikia (laundry)

wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
No. 0753066151
whatsapp 0653506193

Jumamosi, 12 Septemba 2015

UWEKAJI (INSTALLATION) YA UMEME WA NYUMBANI KATIKA UJENZI



Habari za wakati mpendwa msomaji! tunatumaini umzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.
Katika ujenzi kila kazi/kitu kina muda wake mfano huwezi peleka mabati kwenye eneo unalojenga(site) wakati ndiyo kwanza unachimba msingi hivyo basi hata mfumo wa umeme unamuda wake.
Kumbuka: Lengo la kukuwekea mada hii ni kukupa a,b,c.. wewe unayefikiria kujenga au umeshajenga sasa unataka kufanya marekebisho(maintenance).
Wakati wa kuanza kuweka mfumo wa umeme kwenye nyumba.
Baada ya mchoro wa umeme kukamilika (electrical drawing) unaoonesha jinsi mfumo wa umeme utakavyopita kwenye nyumba yako, mfumo huu unaanza kuwekwa katika ngazi zifuatazo;
Mfano wa mchoro wa umeme
  • Kabla ya kupiga lipu(plaster) – Huu ndiyo wakati wa awali kabisa wa kuanza kuweka mfumo wa umeme ambapo mafundi umeme hupitisha mabomba na vibox vya kuwekea switch,socket na distribution box (db).
Jinsi mabomba ya umeme yanavyopitishwa
  • baada ya kufanya umaliziaji(finishing) ya ukuta na kuweka ceiling/gypsum board – wakati huu ndiyo wa mwisho kumalizia kuweka(install) mfumo wa umeme ambapo mafundi umeme wanapitisha nyaya na kupachika taa, switch, socket, nk .
switch

Kumbuka: kama utaratibu huu hautafuatwa basi itabidi mafundi umeme watindue ili kupitisha mabomba wakati umeshafanya umaliziaji (finishing).

Kama upo dar-es-salaam au Dodoma na unashida ya kutatuliwa tatizo lolote linalohusu umeme kwenye nyumba unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba +255753066151 na tutakukutanisha na mafundi umeme wa uhakika

USIPITWE: Endelea kuwa nasi kwa taarifa hizi na nyingine kuhusu ujenzi. 

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Alhamisi, 10 Septemba 2015

JE UNAFAHAMU WAKATI SAHIHI WA KUHAMIA KWENYE NYUMBA KAMA UNAJENGA KIDOGO KIDOGO?



Habari za wakati mpendwa msomaji! Karibu tena kwenye uwanja huru wa kujipatia taarifa na elimu mbadala kwa mambo ya ujenzi.
Ujenzi wa nyumba ya kuishi ni jukumu ambalo kila mtu hulifikiria pale anapofikisha umri fulani wa kujitambua, mara nyingi sio kila mtu anayefikiria hupata fursa ya utekelezaji la hasha hutegemea kipato cha mtu na bajeti yake na ndiyo maana nyumba hutofautiana pia katika ubunifu na malighafi(material) zitakazo tumika.
Kwa ufupi katika ujenzi wa nyumba ya kuishi kuna hatua nne za kuzingatia;
1. Msingi – hii ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa nyumba baada ya kumaliza uchoraji wa ramani na upimaji wa kiwanja na nyumba itakavyokaa (setting out)

2. Upandishaji wa ukuta – hii ni hatua inayofuata baada ya msingi. angalia picha hapo chini

3. Uwezekaji


4. umaliziaji – hii ndiyo hatua ya mwisho na ndiyo hatua ambayo mtu anaweza kuhamia. hatua hii inavitu vingi sana hivyo basi ili uweze kuhamia itakubidi uhakikishe vitu vifuatavyo vya hatua hii umevikamilisha, madirisha, milango(sana sana ya kutokea nje), uwekaji wa mabomba kwa ajili ya umeme na maji, kusakafia(flooring) na kupiga lipu (plaster)

Kumbuka: Lengo la kukuwekea mada hii ni kukupa a,b,c.. wewe unayefikiria kujenga au umeshajenga sasa unataka kuhamia.
Bonyeza maandishi ya blue hapo chini kwa taarifa nyingine zinazoweza kukusaidia
vitu vya kuchunguza kabla hujanunua kiwanja

Kabla hujafikiria kujenga zingatia haya

Vitu 11 vya kuzingatia katika michoro ya jengo ili kupata kibali

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.

kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumamosi, 22 Agosti 2015

HIKI NDIO CHANZO CHA KIPINDUPINDU

Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu za ujenzi.
leo tutaangazia chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ambao umeukumba jamii yetu, Na tatizo hili limekuwa likijirudia takribani kwa kila mwaka nchini kwetu. Tukiwa kama wataalamu wa ujenzi, Tunaliangazia suala hili katika mtazamo nyeti na chanya kabisa.


SeemAndhra - mji uliopangiliwa vyema


Tunaamini huwezi na ni vigumu kupambana na tatizo usilolijua  sababu utashindwa kupata pa kuanzia, Ni dhahiri kuwa hii ni vita ya watu kwa watu na watu na tabia zao.
Ni vita ya watu kwa watu kwa sababu kuna watu ambao wanajua nini kifanyike ili madhara haya yasitokee na kuwa sehemu ya maisha yetu lakini wamekumbatia tatizo hili huku wakifumba macho.



Pili ni vita ya watu na tabia zao kwa maana ya kuwa sehemu kubwa ya jamii yetu imekuwa ikiishi katika mfumo usio rasmi kuona kuwa ni dehemu ya maisha yao kuishi hivyo.

Pengine tuangazie sababu hasa ambayo hupelekea heka heka na mfadhahiko mkubwa kwa jamii na serikali kwa ujumla mara tu kipindupindu kikiibuka.
Sababu ya ugonjwa huu ambao ni aibu kubwa kwa jamii ni uchafu ambao unatokana na kukosekana kwa mpangilio sahihi wa makazi ya watu.




Jamii na serikali kwa ujumla wake ni lazima zitambue kuwa jinsi mwanadamu anavyohitaji kutoa taka mwili vivyo hivyo  nyumba nayo hutoa taka mwili hizo.
Uwepo wa msongamano mkubwa wa makazi ya binadamu ambayo hayajapangiliwa sahihi ndipo utakuta katika mlango wa kuingilia wa nyumba ya mtu X ndio kuna mtaro wa maji taka umepita hapo.
Ni muhimu kufahamu kuwa, kuna maeneo mengi hayajapimwa na serikali na kumekuwa na ujenzi holera wa nyumba za makazi na mamlaka husika zikiwa kimya na cha kushangaza zaidi viongozi wa serikali za mitaa ndio vinara wakubwa wa kuwezesha uuzaji wa maeneo na kuruhusu ujenzi holera.
Yaani watumishi wa serikali hawana elimu tambuzi ya mazingira na athari zake lakini wamekuwa wakipewa majukumu mazito katika kusimamia masula ya kijamii ambayo hawana ujuzi nayo.













NINI KIFANYIKE ?.
Ni muda sahihi kabisa sasa kwa kila mmoja wetu kusema kuwa INATOSHA!! na kujitoa katika mfumo usio rasmi. Pale ambapo serikali inashindwa kunyoosha mkono kumbuka kuwa ni wewe ambaye utaumia na kurudi nyuma kimaendeleo.

  • Epuka ujenzi holera
  • Waone wataalamu wa ujenzi kabla hujaanza kujenga ili kuepuka gharama za kujitakia hapo baadae kama vile kutibu maradhi ya milipuko takribani kila mwaka.
  • Hakikisha unanunua kiwanja kilichopimwa na kimeidhinishwa kuwa ni kiwanja cha makazi ya binadamu.
  • Onana na msanifu majengo akupe ushauri na ramani sahihi kulingana na kiwanja chako kilivyo.

Hivyo UJENZI ELEKEZI TEAM inaihasa jamii kuwa makini na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kujiepusha na adha kama hizi za magonjwa ya milipuko n.k.
KUWA SEHEMU YA MABADILIKO UNAYOTAKA YATOKEE!!!
 KUONANA NA WATAALAMU WETU WA UJENZI (WASANIFU MAJENGO , MAFUNDI N.K) WASILIANA NASI KUPITIA +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Bonyeza hapa kuona jinsi matairi yanavyoweza kutumika kama urembo wa nyumba

USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi












Ijumaa, 21 Agosti 2015

HUU NDIYO MWANZO WA BINADAMU KUISHI KWENYE MAJENGO



Habari za wakati ! pasi na shaka u mzima wa afya, na kama haupo vizuri basi mungu atakujaalia kwa njia atakayopendelea maana mungu hamtupi mja wake.
Kama haujawahi kufatilia historia za mwanzo wa binadamu kuishi kwenye majengo ipo hivi;
Katika miaka ya 3500BC – 324BC (yaani kabla ya kuzaliwa yesu) watu walioanza mfumo wa kujenga walikuwa Wamisri na walikuwa wakijenga kwa madhumuni ya kuhifadhi mwili wa mfalme (FARAO) pale atakapo fariki dunia.
Mtu aliyebuni wazo hili kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri mkuu na aliitwa IMHOTEP. Cheo cha uwaziri mkuu alipewa na FARAO kwa sababu ya uwezo wake wa kujua mambo mengi kama vile uchongaji, kujenga, kutibu na kuongoza.
Muhimu : kujua zaidi historia ya imhotep endelea kutembelea mtandao huu.
Picha zingine
1. Pyramid

2. Great sphinx
3. Hekalu (temple) ya Horus

4. Hekalu la abu simbel

5. picha ya pyramid kwa ndani

Bonyeza maandishi ya blue hapo chini kupata historia nyingine kuhusu ujenzi


USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
 
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumapili, 16 Agosti 2015

USHAURI KWA WALE WANAOTAKA KUJENGA NYUMBA KWENYE KIWANJA KILICHOPO KWENYE MUINUKO



Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi! Lengo letu ni kuhakikisha unaendelea kutembelea mtandao huu kwa kujifunza mambo mbalimbali ya ujenzi
Katika ujenzi kiwanja ni kipande cha eneo ambacho hutumika kwa kujenga majengo mbalimbali. viwanja hutofautiana  kutoka eneo moja hadi lingine kulingana na sura ya eneo husika kama vile bondeni, milimani na tambarare.
Katika viwanja vilivyopo kwenye maeneo yaliyoinuka hususani milimani ujenzi wake huwa tofauti katika msingi(foundation) tofauti na maeneo mengine.
Kuna vitu viwili vya kuzingatia kwa wale wanaotaka kujenga kwenye viwanja vilivyopo kwenye miinuko (slope).
1. Kujenga kwa ngazi(steps) – hii ni aina ya kujenga kwa kufuata usawa (level) ya vieneo vinavyounganisha eneo zima.


2. Kujenga kwa kuchimba/kujaza – hii ni aina ya ujenzi ambayo wajenzi huchimba/kujaza udongo kwa lengo la kusawazisha kisha kuendelea na ujenzi.

Muhimu: Unapofikiria kutengeneza ramani ya kujenga ni vyema kuzingatia hili kwa sababu unaweza kuwa na ramani nzuri lakini isijengeke kwenye kiwanja chako.

Kujifunza zaidi kuhusu viwanja bonyeza maandishi ya blue hapo chini



USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Jumatano, 12 Agosti 2015

PICHA ZA MAUA YA UREMBO YANAYOPENDEZESHA UKUTA



Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi…!
Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia wataalamu mbalimbali wa ujenzi wamekuwa wakifanya vitu tofauti tofauti ili kupendezesha zaidi, kurahisisha na kupunguza gharama za ujenzi.
Hapa tumekuwekea picha zinazoonesha maua ya urembo maalumu yaliyobandikwa kwa kutumia roller kwenye karatasi za ukuta (wallpaper) na mbao.




Kujifunza vitu vingine kwa picha bonyeza maandishi ya blue hapo chini



USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
Namba ya simu: +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506