Jumapili, 16 Agosti 2015
USHAURI KWA WALE WANAOTAKA KUJENGA NYUMBA KWENYE KIWANJA KILICHOPO KWENYE MUINUKO
Je Umeipenda Hii Habari?
Habari za wakati mpendwa
msomaji wa makala hizi za ujenzi! Lengo letu ni kuhakikisha unaendelea
kutembelea mtandao huu kwa kujifunza mambo mbalimbali ya ujenzi
Katika ujenzi kiwanja ni
kipande cha eneo ambacho hutumika kwa kujenga majengo mbalimbali. viwanja
hutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine kulingana na sura ya eneo husika
kama vile bondeni, milimani na tambarare.
Katika viwanja vilivyopo kwenye
maeneo yaliyoinuka hususani milimani ujenzi wake huwa tofauti katika
msingi(foundation) tofauti na maeneo mengine.
Kuna vitu viwili vya
kuzingatia kwa wale wanaotaka kujenga kwenye viwanja vilivyopo kwenye miinuko
(slope).
1. Kujenga kwa ngazi(steps) –
hii ni aina ya kujenga kwa kufuata usawa (level) ya vieneo vinavyounganisha eneo
zima.
2. Kujenga kwa kuchimba/kujaza
– hii ni aina ya ujenzi ambayo wajenzi huchimba/kujaza udongo kwa lengo la
kusawazisha kisha kuendelea na ujenzi.
Muhimu:
Unapofikiria kutengeneza ramani ya kujenga ni vyema kuzingatia hili kwa
sababu unaweza kuwa na ramani nzuri lakini isijengeke kwenye kiwanja
chako.
Kujifunza zaidi kuhusu viwanja bonyeza maandishi ya blue hapo chini
USIPITWE!!
Endelea kuwa nasi kwa taarifa
nyingine kuhusu ujenzi.
kwa ushauri/maoni/swali
wasiliana nasi kupitia
email: ujenzielekezi04@gmail.com
Namba ya simu: +255 753 066
151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
1 COMMENT
26 Novemba 2019, 03:30
Naomba kupata mwongozo najua kuchora raman kwenye karatasi lakini sijui kuchora kwenye computer .idea ninayo lakini sijui nianzie wapi ?
Chapisha Maoni