Jumamosi, 22 Agosti 2015
Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu za ujenzi.
leo tutaangazia chanzo cha ugonjwa wa kipindupindu ambao umeukumba jamii yetu, Na tatizo hili limekuwa likijirudia takribani kwa kila mwaka nchini kwetu. Tukiwa kama wataalamu wa ujenzi, Tunaliangazia suala hili katika mtazamo nyeti na chanya kabisa.
SeemAndhra - mji uliopangiliwa vyema |
Tunaamini huwezi na ni vigumu kupambana na tatizo usilolijua sababu utashindwa kupata pa kuanzia, Ni dhahiri kuwa hii ni vita ya watu kwa watu na watu na tabia zao.
Ni vita ya watu kwa watu kwa sababu kuna watu ambao wanajua nini kifanyike ili madhara haya yasitokee na kuwa sehemu ya maisha yetu lakini wamekumbatia tatizo hili huku wakifumba macho.
Pili ni vita ya watu na tabia zao kwa maana ya kuwa sehemu kubwa ya jamii yetu imekuwa ikiishi katika mfumo usio rasmi kuona kuwa ni dehemu ya maisha yao kuishi hivyo.
Pengine tuangazie sababu hasa ambayo hupelekea heka heka na mfadhahiko mkubwa kwa jamii na serikali kwa ujumla mara tu kipindupindu kikiibuka.
Sababu ya ugonjwa huu ambao ni aibu kubwa kwa jamii ni uchafu ambao unatokana na kukosekana kwa mpangilio sahihi wa makazi ya watu.
Jamii na serikali kwa ujumla wake ni lazima zitambue kuwa jinsi mwanadamu anavyohitaji kutoa taka mwili vivyo hivyo nyumba nayo hutoa taka mwili hizo.
Uwepo wa msongamano mkubwa wa makazi ya binadamu ambayo hayajapangiliwa sahihi ndipo utakuta katika mlango wa kuingilia wa nyumba ya mtu X ndio kuna mtaro wa maji taka umepita hapo.
Ni muhimu kufahamu kuwa, kuna maeneo mengi hayajapimwa na serikali na kumekuwa na ujenzi holera wa nyumba za makazi na mamlaka husika zikiwa kimya na cha kushangaza zaidi viongozi wa serikali za mitaa ndio vinara wakubwa wa kuwezesha uuzaji wa maeneo na kuruhusu ujenzi holera.
Yaani watumishi wa serikali hawana elimu tambuzi ya mazingira na athari zake lakini wamekuwa wakipewa majukumu mazito katika kusimamia masula ya kijamii ambayo hawana ujuzi nayo.
NINI KIFANYIKE ?.
Ni muda sahihi kabisa sasa kwa kila mmoja wetu kusema kuwa INATOSHA!! na kujitoa katika mfumo usio rasmi. Pale ambapo serikali inashindwa kunyoosha mkono kumbuka kuwa ni wewe ambaye utaumia na kurudi nyuma kimaendeleo.
- Epuka ujenzi holera
- Waone wataalamu wa ujenzi kabla hujaanza kujenga ili kuepuka gharama za kujitakia hapo baadae kama vile kutibu maradhi ya milipuko takribani kila mwaka.
- Hakikisha unanunua kiwanja kilichopimwa na kimeidhinishwa kuwa ni kiwanja cha makazi ya binadamu.
- Onana na msanifu majengo akupe ushauri na ramani sahihi kulingana na kiwanja chako kilivyo.
Hivyo UJENZI ELEKEZI TEAM inaihasa jamii kuwa makini na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ili kujiepusha na adha kama hizi za magonjwa ya milipuko n.k.
KUWA SEHEMU YA MABADILIKO UNAYOTAKA YATOKEE!!!
KUONANA NA WATAALAMU WETU WA UJENZI (WASANIFU MAJENGO , MAFUNDI N.K) WASILIANA NASI KUPITIA +255 753 066 151, +255 655 699 342, +255 714 835 965
Bonyeza hapa kuona jinsi matairi yanavyoweza kutumika kama urembo wa nyumba
USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi
Ijumaa, 21 Agosti 2015
Habari za wakati ! pasi na shaka u mzima wa afya, na kama haupo vizuri basi mungu atakujaalia kwa njia atakayopendelea maana mungu hamtupi mja wake.
Kama haujawahi kufatilia historia za mwanzo wa binadamu kuishi kwenye majengo ipo hivi;
Katika miaka ya 3500BC – 324BC (yaani kabla ya kuzaliwa yesu) watu walioanza mfumo wa kujenga walikuwa Wamisri na walikuwa wakijenga kwa madhumuni ya kuhifadhi mwili wa mfalme (FARAO) pale atakapo fariki dunia.
Mtu aliyebuni wazo hili kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri mkuu na aliitwa IMHOTEP. Cheo cha uwaziri mkuu alipewa na FARAO kwa sababu ya uwezo wake wa kujua mambo mengi kama vile uchongaji, kujenga, kutibu na kuongoza.
Muhimu : kujua zaidi historia ya imhotep endelea kutembelea mtandao huu.
4. Hekalu la abu simbel
5. picha ya pyramid kwa ndani
Jumapili, 16 Agosti 2015
Jumatano, 12 Agosti 2015
Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia wataalamu mbalimbali wa ujenzi wamekuwa wakifanya vitu tofauti tofauti ili kupendezesha zaidi, kurahisisha na kupunguza gharama za ujenzi.
Hapa tumekuwekea picha zinazoonesha maua ya urembo maalumu yaliyobandikwa kwa kutumia roller kwenye karatasi za ukuta (wallpaper) na mbao.
Jumatano, 5 Agosti 2015
UTANGULIZI:
Dari imekuwa ni sehemu amabayo inasahaulika sana katika ujenzi wa nyumba zetu kwa maana ya kuwa inapewa angalizo kidogo sana.
Lakini umaliziaji mzuri wa Dari huweza kuzidisha uzuri wa nyumba yako.
Dari imekuwa ikificha bomba za umeme na huduma nyingi ili kuondoa uzia kwa wakazi wa nyumba husika na kuwapa muonekano mzuri.
Ili kuweza kupata faida zote za Dari ni vyema kumpata fundi mzuri na mtaalamu mzuri au msanifu mzuri wa majengo wataoweza kusimamia kazi hiyo kwa ufanisi unaotakiwa.
Hivyo basi ni vyema tuangazie namna mbalimbali za kupendezesha au kumalizia vizuri Dari la nyumba yako.
NAMNA MBALIMBALI ZA UMALIZIAJI WA DARI:
Ni vizuri ukabaini kwanza ni nini unataka kupata au muonekano gani unataka kuupata kwa kulingana na wapi Dari lako linatarajiwa kujengwa, kwa maana ya kuwa kama ni sebuleni au vyumbani,au jikoni n.k.
Jumamosi, 1 Agosti 2015
Katika ujenzi wa jengo kuna hatua mbalimbali mpaka jengo kukamilika. Hapa tuguse upande wa umaliziaji wa ndani (interior finishing) katika majengo ya kuishi (residential house).