+255 753 066 151

ujenzielekezi04@gmail.com

Ubungo Kibangu at Kinondoni Dar-es-salaam Tanzania

Alhamisi, 30 Aprili 2015

hivi ndiyo vitu vya msingi kuwepo kwenye chumba cha kulala (bedroom)

1

Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi, ni matumaini yetu kwamba umzima wa afya.

Leo tunataka tukupitishe kwenye vitu vinavyohitajika hasa kuwepo ndani ya chumba kiitwacho chumba cha kulala(bedroom). Kabla hatujakueleza ni vitu gani vya msingi tupate kujua ni kwanini unatakiwa uvijue.

1. kujua nafasi inayohitajika-watu wengi hujua kubuni nafasi ni kazi ya wasanifu majengo/ wachora ramani tu, lakini jua kwamba huyu mchora ramani anahitaji kujua pia unataka nini kiwepo ndani ili aweze kubuni kwa ufanisi. Na ndiyo maana unakuta vyumba vya kulala vinatofautiana ukubwa nyumba hadi nyumba au chumba hadi chumba.

2. Usiboreke- mara nyingi hali ya kuboreka hutokea pale mtu anapoona nafasi haitoshi, au rangi ya chumba inamkifu (hajapendezwa nayo), hakuna hewa ya kutosha na nk.

3. kupanda thamani- Hii hutokea kwa nyumba nzima. mfano nyumba ambayo vyumba vyake vimepangiliwa vizuri gharama yake ya kuiuza ni kubwa ukilinganisha na nyumba ambayo vyumba vyake havikupangiliwa vizuri.

Vitu vya msingi kuwepo kwenye chumba cha kulala (bedroom)

  1. Kitanda
  2. kimeza/kikabati cha kitanda (bedside table)
  3. kabati/meza ya kujipambia (dressing table)
  4. viti viwili au kimoja cha kukalia
  5. meza/kabati la TV

2

1 COMMENT

Lightness Kweka alisema ...
30 Juni 2018, 01:04

Naomba kufahamu gharama za wiring wa chumba kimoja


Chapisha Maoni

Popular

All Rights Reserved UJENZI ELEKEZI | Mtengenezaji wa BLOGG CHIKULO +255657103506 | +255753103506