Alhamisi, 30 Aprili 2015
Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala zetu zinazohusu ujenzi, ni matumaini yetu kwamba umzima wa afya.
Leo tunataka tukupitishe kwenye vitu vinavyohitajika hasa kuwepo ndani ya chumba kiitwacho chumba cha kulala(bedroom). Kabla hatujakueleza ni vitu gani vya msingi tupate kujua ni kwanini unatakiwa uvijue.
1. kujua nafasi inayohitajika-watu wengi hujua kubuni nafasi ni kazi ya wasanifu majengo/ wachora ramani tu, lakini jua kwamba huyu mchora ramani anahitaji kujua pia unataka nini kiwepo ndani ili aweze kubuni kwa ufanisi. Na ndiyo maana unakuta vyumba vya kulala vinatofautiana ukubwa nyumba hadi nyumba au chumba hadi chumba.
2. Usiboreke- mara nyingi hali ya kuboreka hutokea pale mtu anapoona nafasi haitoshi, au rangi ya chumba inamkifu (hajapendezwa nayo), hakuna hewa ya kutosha na nk.
3. kupanda thamani- Hii hutokea kwa nyumba nzima. mfano nyumba ambayo vyumba vyake vimepangiliwa vizuri gharama yake ya kuiuza ni kubwa ukilinganisha na nyumba ambayo vyumba vyake havikupangiliwa vizuri.
Vitu vya msingi kuwepo kwenye chumba cha kulala (bedroom)
- Kitanda
- kimeza/kikabati cha kitanda (bedside table)
- kabati/meza ya kujipambia (dressing table)
- viti viwili au kimoja cha kukalia
- meza/kabati la TV
Jumatatu, 13 Aprili 2015
Mpendwa msomaji wa makala zetu tunaomba radhi kwa kuwa kimya kipindi kirefu kutokana na majukumu ya hapa na pale, na kwasasa tumejipanga vizuri kukuhabarisha na kukuelimisha kuhusu ujenzi karibu sana na karibu tena.
Nyavu (wire mesh) ni moja ya malighafi zinazotumika kwenye ujenzi wa majengo mbalimbali kama nyumba ya kuishi (milangoni na madirishani), na nyumba za wanyama/ndege wanaofugwa kama vile kuku, bata, kanga, N.K . Nyavu zipo za aina nyingi kulingana na ukubwa wa matundu yake
Upatikanaji
Nyavu hupatikana kwenye maduka yanayouza vifaa vya ujenzi, pia unaweza kukuta hata kwenye maduka ya vitu vigumu (hardware).
Ubora
Nyavu hutofautiana ubora kulingana na sehemu/kampuni iliyotengenezwa hivyo basi ni vizuri kununua nyavu ambazo mfuko wake unalebo na kwenye maduka yanayotambulika (usisahau risiti). Ni vizuri zaidi kutumia nyavu zilizopakwa rangi kwa ubora zaidi
Uwekaji na utunzaji
Nyavu ni kitu kinachoathirika sana na kutu hivyo basi hazitakiwi kuwekwa chini(kwenye sakafu) au sehemu yenye unyevu unyevu mfano nje ya nyumba.
Gharama yake kwa sasa
Jina | Gharama (Tsh)/= |
nyavu ngogo(za mbu) | 3000-4500 kipande(piece) |
zinazofatia kwa ukubwa | 5000-7000 kipande(piece) |
kumbuka:gharama zinabadilika kutokana na eneo husika, hizi ni gharama kwa Dodoma mjini.
kwa maelezo zaidi au ushauri tuandikie kupitia email yetu ujenzielekezi04@gmail.com au piga simu namba +255653506193